THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

VETA kuanzisha kozi ya Utalii wa Kitamaduni

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii,MIKUMI .
 
Mamlaka ya Elimu na mafunzo ya Ufundi stadi (VETA) kupitia chuo cha VETA Mikumi inatarajia kuanzisha kozi ya utalii wa kitamaduni ili kuwafundisha watanzania tamaduni ,mila na desturi kuulinda utamaduni wetu , ambao unaonekana kupotea kadri teknolojia inavyozidi kukua kila siku. 

Akizungumza na waandishi wa habari walipotemebelea chuo hicho Cha VETA Mikumi, Mkuu wa chuo hicho Christopher Ayo amesema kuwa uamuzi huo umetokana na sekta ya utalii kuendelea kukua mwaka hadi mwaka huku jamii ikionekana kusahahu uhasilia wa tamaduni mbalimbali za kitanzania . 

Amesema utamaduni ukitumika ipasavyo unaweza kuchangia ukuaji wa sekta ya utalii pamoja na uchumi nchini kutokana na ukweli kwamba nchi nyingi duniani zimeweza kulinda utamaduni kuweza kukuza uchumi wao.
 
Amesema chuo chake kwa kushirikiana na Chuo cha NOVA Scotia Community College cha nchini Canada kinaandaa kozi hiyo itakayowezesha watanzania kujifunza kwa undani kuhusu utamaduni wao kama vile ngoma, vyakula vya asili ,sanaaa na historia ya makabila mbalimbali. 

Ayo amesema maandalizi ya kuanzisha kozi hiyo yapo kwenye hatua za mwisho na kwamba kuanzia Januari, 2017 masomo yataanza kutolewa.
Aidha mkuu huyo amesema walimu watano watakaofundisha masomo hayo wameshaandaliwa na kupatiwa mafunzo nchini Canada jinsi ya kutumia technologia katika kufundisha na kuandaa mitaala. 

Ayo amesema VETA Mikumi itaendelea kutoa mafunzo kwa jamii inayowazunguka katika kuwaandaa vijana katika soko la ajira kwa kujiajiri au kuajiriwa na kuweza kuendesha maisha yao na kuchangia pato la taifa.
 

Ametoa rai kwa vijana wa mikumi na maeneo ya mengine ya Mkoa wa Morogoro kuchangamkia fursa za mafunzo zilizopo chuoni hapo ili kuweza kuwa sehemu ya wataalam watakaohudumia viwanda vitakavyojengwa kutokana na serikali ya awamu ya tano ya Rais Dk. John Pombe Magufuli kuweka msisitizo wa kuhakikisha nchi inakuwa ya viwanda.

Mwalimu wa Ufundi Mitambo wa Chuo cha VETA Mikumi, Peris Shao, akizungumza na waandishi wa habari juu maendeleo ya chuo hicho katika utoaji wa mafunzo ya ufundi Stadi.
Wanafunzi wakiwa katika karakana ya ufundi Mitambo wakiendelea na mafunzo ya vitendo katika Chuo cha Mikumi.

Mwalimu wa Chuo cha VETA Mikumii, James Maungu akitoa maelezo kwa waandishi wa habari walipotembelea karakana ya ufundi huo.
Mwanafunzi wa mwaka wa mwisho wa Chuo cha VETA Mikumi wakiwa katika mafunzo ya vitendo karakana ya ufundi wa Magari. 


Kuna Maoni 2 mpaka sasa.

  1. A very good move. Utalii wa kiutamaduni, utasaidia kuzalisha maelfu ya ajira kwa vijana

  2. Professionalism in tour guiding is important, tell your friends.