THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

VIONGOZI MBALIMBALI WAOMBOLEZA KIFO SPIKA MSTAAFU WA BUNGE, MH. SAMUEL SITTA


 Mwenyekiti  wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida akisaini kitabu cha maombolezo, wakati alipofika nyumbani kwa Marehemu Mh. Samuel Sitta aliekuwa Spika wa Bunge na Waziri Mwandamizi katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, aliefariki leo Novemba 7, 2016 huko nchini Ujerumani. Msiba upo Nyumbani kwa Marehemu, Masaki jijini Dar es salaam.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda (wa pili kulia) akiwa katika mazungumzo na baadhi ya viongozi pamoja ndugu wa Marehemu Mh. Samuel Sitta aliekuwa Spika wa Bunge na Waziri Mwandamizi katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, aliefariki leo Novemba 7, 2016 huko nchini Ujerumani.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kinondoni, Salum Madenge akisaini kitabu cha Maombolezo cha aliekuwa Spika wa Bunge na Waziri Mwandamizi katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, aliefariki leo Novemba 7, 2016 huko nchini Ujerumani.
Sehemu ya ndugu wa Marehemu wakiwa nyumbani hapo.