Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

LIGI kuu ya Tanzania bara inatarajia kuendelea kutimua vumbi hapo kesho katika viwanja sita tofauti hapa nchini ikiwa kila timu ikihitaji ushindi ili kujiweka kwenye nafasi nzuri katika msiamamo wa ligi.

Mkoani Mbeya,Mbeya City itakuwa nyumbani kuwakaribisha mabingwa watetezi wa kombe hilo timu ya soka ya Yanga katika mchezo unaotarajiwa kupigwa kwenye uwanja wa Sokoine mkoani humo.

Stand United ya mkoani Shinyanga mara baada ya kukamilisha mchezo wao wa juzi dhidi ya JKT RUVU uliochezwa kwenye uwanja Mabatini itakuwa nyumbani kuwakaribisha wekundu wa Msimbazi timu ya Simba.

 Toto Africa watawakaribisha Azam Fc katika dimba la CCM kirumba na kila mmoja akiwa na kumbukumbu ya ushindi katika michezo yao iliyopita, Ruvu shooting wataikaribisha African Lyon kwenye Uwanja wa Mabatini.

Majimaji baada ya kupoteza mchezo wao dhidi ya Mbeya City mwishoni mwa wiki watavaana na JKT Ruvu katika Uwanja wa Majimaji Songea huku Tanzania Prisons watakuwa wageni kwenye Uwannja wa Nangwanda Sijaona kuvaana na Ndanda.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...