THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

VIWANJA VYA MICHEZO KUJENGWA KATA YA ENGUTOTO


Na Woinde Shizza,Arusha

WANANCHI kutoka kata ya Engutoto jijini hapa,wanatarajiwa kutimiza ndoto zao za muda mrefu juu ya ukosefu wa viwanja baada ya mfadhili kujitokeza kuwajengea.

Mfadhili huyo Hans Paul kupitia kampuni ya Dharam Singh Hanspaul & Son ltd alisema hayo mbele ya mkuu wa mkoa Arusha kuwa katika kutimiza adhma ya serikali kusaidia maendeleo ya michezo kwa vijana amejitolea kujenga viwanja viwili vya michezo.

“Viwanja tutakavyojenga ni kwa mpira wa miguu na mpira wa Netiboli na vinatarajiwa kugharimu kiasi cha shilingi milioni 30 fedha za kitanzania na tunatarajia kuanza ujenzi huo ifikapo mwanzoni mwa mwaka 2017,”Alisema Paul.

Alisema kuwa lengo kuu la kujenga viwanja ni katika kuwawezesha vijana wapate muda wa kujihusiha na michezo ili kuepukana na tabia hatarishi ambazo zingeharibu ndoto za maisha yao.

Baahi ya wakazi wa kata hiyo wakizungumzia neema watakayoipata kutoka kwa mfadhili huyo walisema “Ni jambo la kupongeza kwani vijana wengi wamekuwa hawana mahali pa kufanya mazoezi na kwa hali hii itasidia sasa kuanza kuona vipaji vya michezo katika kata hii.” Alisema mmoja wa wakazi hao.

Kwa upande wake mkuu wa mkoa Arusha Mrisho Gambo alisema juhudi alizozifanya mfadhili huyo katika sekta ya michezo ni jambo la heri ambalo linatakiwa liwe mfano kwa wadau wengine katika kusaidia kuinua michezio katika jamii sambamba na kuwa michezo ni moja ya ajira kwa Vijana .

Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo(kwanza kulia) akizungumza na wadau wa maendeleo Bw. Hans Paul(pili kulia) ambaye amehaidi kujenga viwanja vya michezo ndani ya kata ya Engutoto na Bw. Jagjit Aggarwal