Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya juu kote nchini wametakiwa kutumia muda mwingi kujisomea na kuepuka kujiingiza kwenye vitendo vya vurugu , migomo na maandamano yasiyo na tija kwa taifa ambayo yamekuwa yakiwapunguzia ufanisi katika masomo yao.

Wito huo umetolewa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Suzan Kaganda wakati akizungumza na Jumuiya ya wanataaluma wa Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam (CBE) kwenye kongamano la 3 lililowakutanisha wahitimu wa chuo hicho mwaka huu, wanataaluma waliopo na wale waliowahi kusoma katika chuo hicho (CBE Alumni Association) na wadau mbalimbali jijini Dar es salaam.

Akiwa mgeni rasmi katika kongamano hilo na mmoja wa wahitimu wa siku nyingi wa chuo hicho Kamanda Suzan Kaganda amesema wanafunzi wa vyuo vya Elimu ya juu wanapaswa kutambua kuwa elimu wanayoipata katika vyuo hivyo sio kwa ajili ya manufaa yao binafsi bali ni kwa manufaa ya taifa zima hivyo wanatakiwa kuwa makini na kuwa mfano wa kuigwa katika jamii.

“Naomba nisisitize kuwa elimu mliyoipata na mnayoendelea kuipata chuoni hapa sio kwa ajili ya manufaa yenu binafsi bali ni kwa ajili ya manufaa ya taifa, wakati mwingine mnapoteza muda mwingi pindi mnapojiingiza kwenye migomo na maandamano barabarani kushindana na Serikali, muda ambao mgeutumia kujisomea ninyi wenyewe” Amesisitiza Kamanda Suzan.

Wanafunzi wa CBE, Adam Luhalala (kushoto) na Petro Nchimbi wakifanya ukaguzi wa Mashine ya kutengeneza vipuri mbalimbali vinavyotumika kwenye mashine za viwandani na Magari ndani ya Karakana ya Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) jijini Dar es salaam.
ahitimu wa chuo CBE mwaka huu, wanataaluma waliopo na wale waliowahi kusoma katika chuo hicho (CBE Alumni Association) na wadau mbalimbali waliohudhuria kongamano la 3 la chuo hicho jijini Dar es salaam.
Mwanafunzi wa Mwaka wa 2 katika fani ya Vipimo Mathew Kaizilege akitoa ufafanuzi kuhusu mashine ya kuchonga vipuri kwa wanafunzi wa shule ya Sekondari Jangwani walioitembelea Karakana ya Vipimo ya CBE jijini Dar es salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...