Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii 

WAKIMBIZI wamekuwa wakiishi maisha ya kambini  kutokana na sheria pamoja na mikataba hali ambayo imesababisha  kukosa fursa ya  kuzalisha katika taifa walilopo.

Akizungumza na waandishi katika mafunzo yaliyoandaliwa na Asylum Access, Mhadhili wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,  Dk. Juliana Masabo amesema kuwa Tanzania ni nchi ambayo imekuwa ikipata wakimbizi ambao wanaishi katika makambi lakini kutokana na sheria ya wakimbizi  inaelekeza kuishi katika mazingira hayo bila kujishughulisha na uzalishaji  wowote.

Amesema  wakimbizi wana haki sawa kama binadamu wengine hivyo sheria zinahitaji kufanyiwa  maboresho kutokana na mazingira yaliyopo, wanatakiwa kuangaliwa kuwa sehemu ya watu ambao wanaweza kuzalisha 

Dk. Juliana amesema kuwa kuna watu ni wataalam lakini wamekuwa wakimbizi lakini hawawezi kuajiliwa katika taifa walilopo kutokana na sheria kuwabana ya ukimbizi hivyo utaalam walio  nao unabaki katika makambi usio wa  uzalishaji.

 Nae Wakili na Mtetezi wa Haki za Wakimbizi, Veronica Hollela amesema kuwa kunahitajika kufanyika kwa uboreshaji wa sheria ya  wakimbizi ili kuweza kuishi kwa huru na kufanya kazi kama raia wengine na kuwa faida ya nchi kuongeza uchumi.

Veronica amesema maisha ya wakimbizi ni magumu kutokana na kukaa sehemu moja ambayo hawana uzalishaji na kuishi kwa kutegemea misaada.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Boniventure Rutinwa akitoa mafunzo kwa waandishi wa habari juu kutoa taarifa zinazohusu wakimbizi na changamoto zao , mafunzo hayo yameandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la Aslum Access yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Juliana Masabo akitoa mafunzo kwa waandishi wa habari juu ya sheria zinazohuusu wakimbizi mafunzo hayo yameandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la Aslum Access yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
picha wa pamoja ya wakufunzi wa mafunzo wakiwa katika picha ya pamoja na waandishi wa habari walioshiriki mafunzo juu ya wakimbizi mafunzo hayo yameandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la Aslum Access yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...