THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

WABUNGE WA BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI WATEMBELEA IDARA YA UHAMIAJI


Kaimu Kamishna Utawala na Fedha wa Idara ya Uhamiaji, Naibu Kamishna Abbas Irovya, akizungumza wakati wa mkutano na Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki waliotembelea idara ya Uhamiaji kujadili shughuli zinazofanywa na idara hiyo, ikiwa ni ziara yao ya kujifunza mambo mbalimbali yanayohusiana na nchi za Afrika Mashariki ikiwemo suala la pasi za kusafiria katika nchi hizo.Ziara hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam.( Picha na Abubakari Akida) 
Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Abdullah Mwinyi akizungumza wakati wa mkutano na Wakuu wa Idara ya Uhamiaji(hawapo pichani).Wabunge hao walitembelea idara hiyo kujifunza shughuli mbalimbali zinazofanywa ikiwemo utoaji wa pasi za kusafiria katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki. Kushoto ni Katibu wa Wabunge wa Afrika Mashariki Twaha Taslima. Mkutano huo umefanyika jijini Dar es Salaam. (Picha na Abubakari Akida).
Mwenyekiti wa Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki Tawi la Tanzania, Makongoro Nyerere(kulia) akizungumza wakati wa mkutano na Wakuu wa Idara ya Uhamiaji(hawapo pichani).Wabunge hao walitembelea idara hiyo kujifunza shughuli zinazofanywa na idara hiyo . Wengine ni Wabunge Shyrose Bhanji(kulia) na Angela Kizigha(kushoto). Mkutano huo umefanyika jijini Dar es Salaam.( Picha na Abubakari Akida) 
Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Shyrose Bhanji akizungumza wakati wa mkutano na Wakuu wa Idara ya Uhamiaji(hawapo pichani).Wabunge hao walitembelea idara hiyo kujifunza shughuli zinazofanywa na idara .Kulia ni Mbunge Makongoro Nyerere na Kushoto ni Angela Kizigha.Mkutano huo umefanyika jijini Dar es Salaam. 
Kaimu Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Victoria Lembeli akizungumza wakati wa mkutano na Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki waliotembelea idara hiyo, ikiwa ni ziara yao ya kujifunza shughuli mbalimbali zinazofanywa na idara hiyo ikiwemo suala la pasi za kusafiria katika nchi hizo.Ziara hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam.
Kaimu Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Victoria Lembeli(wanne kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki Tawi la Tanzania baada ya kutembelea Makao Makuu ya Idara hiyo katika kujifunza mambo mbalimbali yanayofanywa na idara .Watatu kulia ni Mwenyekiti wa Wabunge wa Tanzania katika Bunge hilo, Makongoro Nyerere.Ziara hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam.(Picha na Abubakari Akida)