Na Antony John,Globu ya Jamii.

Wadau wa Soko la Pamoja la Afrika Mashariki wamefanya mkutano leo Jijini Dar es salaam wakishirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi Nchini (TPSF) ili kujadili utekelezaji wa Soko hilo.
 

Akizungumza katika Mkutano huo,Mkurugenzi wa Huduma kwa Wanachama wa TPSF,Louis Accaro amesema Afrika Mashariki ina Nchi sita zilizokubaliana kuwepo na soko la pamoja lengo likiwa ni kuondoa vikwazo vya kibiashara.

"Katika utekelezaji wa soko hili,hasa kuangalia vikwazo ambavyo vinazuia biashara isifanyike mfano kutoa mzigo kutoka nchi moja hadi nyingine na vikwazo vingine vya kibiashara",amesema Accaro.

Pia Mtaalamu wa Huduma za biashara wa Soko hilo la pamoja,Octavian Kinyiro amesema kuwa tukiondoa vikwazo mbalimbali vya kibiashara kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki,watu wengi watakuja kufanya biashara katika Soko hili.

"Zamani watanzania walikuwa hawaruhusiwi kuwekeza nchi nyingine, sheria zetu zilikuwa haziruhusu lakini kwa sasa zimeondolewa ili wapate fursa zakuwekeza nje ya nchi",amesema Kinyiro.

Mkurugenzi wa Huduma kwa Wanachama wa TPSF,Louis Accaro akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya kukutana pamoja na wadau mbalimbali kujadili utekelezaji wa Soko la pamoja Afrika Mashariki.
Wadau wa Sekta ya Biashara,Uwekezaji wakiwa katika Mkutano huo wa kujadili masuala mbali mbali ya Soko la pamoja la Afrika Mashariki.
Mtaalamu wa Huduma za biashara wa Soko hilo la pamoja,Octavian Kinyiro akitoa tathmini ya Huduma za Biashara katika Idara ya Biashara,Uwekezaji na Sekta za Uzalishaji katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...