THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

WADAU WAJADILI MAOMBI YA TANESCO KUPANDISHA BEI YA UMEME JIJINI DAR ES SALAAM


Na K-VIS BLOG/KHALFAN SAID
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amewataka wadau wa umeme kujadili maombi ya Shirika la Umeme Nchini TANESCO ya kupandisha bei ya umeme kwa asilimia 18.9 kwa uwazi na bila hofu lakini wakizingatia nia ya Serikali ya awamu ya tano ya kujenga nchi yenye uchumi wa viwanda.

Akifungua majadiliano ya wadau wa Mkoa wa Dar es Salaam, Zanzibar na uongozi wa TANESCO jijini Novemba 23, 2016 kwenye ukumbi wa mikutano wa Mamlaka ya Udhibiti Huduma za Maji na Nishati, (EWURA), kuhusu mapendekezo hayo, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi, (pichani juu), ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa, Paul Makodna alisema, “Rais wetu Mh. Dkt. John Pombe Magufuli, amedhamiria kujenga uchumi wa viwanda ambao utafanikiwa tu endapo tutakuwa na umeme wa uhakika na ulio bora.” Alisema.
 Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Umeme nchini TANESCO, Mhandisi Decklan Mhaiki, akiwasilisha mambi ya shirika hilo ya kupaandishi bei ya umeme kwa asilimia 18.9 wakati wa kikao cha majadiliano baina ya wadau na uongozi wa shirika, kilichoitishwa na Mamlaka ya Udhibiti huduma za Maji na Nishati, (EWURA), na kufanyika jijini Dar es Salaam, Novemba 23, 2016.
 Baadhi ya viongozi wa TANESCO na wadau wakifuatilia mjadala

Aliwataka wadau kusikiliza kwa makini hoja za TANESCO zinazowasukuma kupandisha bei ya umeme, lakini TANESCO nao wanapaswa kusikiliza maoni ya wananchi kuhusu mapendekezo yao.