Na Nathaniel Limu-Singida.

Wafanyabiashara wa kuku wa asili/kienyeji mkoani Singida wamejipatia mapato ya zaidi ya shilingi bilioni 1.8, baada ya kuuza kuku 151,242 katika kipindi cha mwaka jana hadi sasa.

Hayo yamesemwa juzi na kaimu Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji Beatus Choaji wakati akitoa taarifa ya uendelezaji wa kuku wa asili, kwenye kikao cha kamati ya ushauri mkoa (RCC) kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano uliopo kwenye jengo la ofisi ya mkuu wa mkoa mjini hapa.

Chowaji amesema mapato hayo yamepatikana baada ya kuku hao 151,242 kusafirishwa  na kuuzwa nje ya mkoa ikiwemo jijini Dar-es-salaam.“Kuku wa asili wakifungwa vizuri kwa kudhibiti ugonjwa wa mdondo na kuzingatia kanuni za ufugaji bora wanaweza kuleta mabadiliko makubwa na ya haraka ya kipato. Kuku wa asili pia ni lishe bora hususani kwa watoto na akina mama”, ameongeza Choaji.

Ili kuimarisha ufugaji kuku wa asili amesema imependekezwa halmashauri zote zitekeleze mkakati wa kuchanja kuku kwa wakati moja mara tatu kwa mwaka kwa kutumia watoa chanjo wasiokuwa wataalam wa mifugo.
Mwenyekiti wa Kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa na Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew John Mtigumwe akiongoza kikao hicho, kushoto kwake ni Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dokta Angelina Mageni Lutambi, wa kwanza kulia ni Waziri wa Mambo ya ndani Mwigulu Lameck Nchemba na anayefuata ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida Mhe. Martha Mlata.
Mbunge wa Viti maalum CCM Singida Aisharose Matembe akichangia hoja katika kikao cha kamati ya ushauri ya Mkoa wa Singida (RCC). 


Meneja wa SIDO Mkoa wa Singida Shoma Kibende akichangia hoja katika kikao cha kamati ya ushauri ya Mkoa wa Singida (RCC).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...