Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage amewataka wahitimu 1,811 wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) waliotunukiwa stahili zao katika Fani mbalimbali kwa mwaka 2016 kuchangamkia fursa za ajira zilizopo nchini kwa kuanzisha makampuni na viwanda vidogo vidogo vitakavyowawezesha kujiajiri na kuajiri wengine. 
 Akizungumza katika mahafali ya 51 ya chuo hicho jijini Dar es salaam Mhe.Mwijage amesema kuwa makampuni na viwanda vidogo vidogo watakavyoanzisha vitatumika kuzalisha bidhaa mbalimbali zenye ubora ambazo zitauzwa kote duniani hivyo kukuza uchumi wa nchi na kuwapatia ajira ya uhakika. 
 Amesema Serikali ya Tanzania inapenda kuwaona Wawekezaji wengi wa Kitanzania wakiingia na kuwekeza kwenye rasilimali mbalimbali zilizopo nchini Tanzania badala ya kuwaachia wageni kwa kuwa inao wasomi waliobobea kwenye fani ya biashara pamoja na ujasiriamali. 
 " Taifa letu limebarikiwa kuwa na fursa nyingi za kujiletea maendeleo, Serikali ingependa kuona wawekezaji wengi wa Kitanzania wakiwekeza kwenye rasilimali zilizopo kwa mfano tunayo gesi, madini, kilimo na na rasilimali nyinginezo nyingi" Amesisitiza Mhe.Mwijage. 
 Amefafanua kuwa Serikali itaendelaea kuwekeza kwenye Elimu ya Biashara kuwawezesha wananchi wengi zaidi kujiajiri na kuajiriwa katika sekta binafsi hasa Biashara.

 Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage akizungumza na wahitimu 1,811 wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) waliotunukiwa stahili zao katika Fani mbalimbali kwa mwaka 2016 wakati wa Mahafali ya 51 ya chuo jijini Dar es salaam.
 Mwenyekiti wa Bodi ya CBE Prof.Mathew Luhanga akizungumza na wahitimu wa Chuo hicho wakati wa Mahafali ya 51 jijini Dar es salaam.
 Wahitimu wa Chuo cha Elimu ya Biashara CBE wakivaa kofia zao mara baada ya kutunukiwa Shahada zao katika fani mbalimbali wakati wa mahafali ya 51 ya Chuo cha Elimu ya Biashara jijini Dar es salaam.
  Wahitimu wa Chuo cha Elimu ya Biashara CBE wakivaa kofia zao mara baada ya kutunukiwa Shahada zao katika fani mbalimbali wakati wa mahafali ya 51 ya Chuo cha Elimu ya Biashara jijini Dar es salaam.
Baadhi ya Wahitimu wa CBE fani ya wakifurahia mara baada ya kutunukiwa Shahada zao mgeni Rasmi Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mijage. Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...