Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii, Mikumi

Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Adam Mgoyi amewaasa  wahitimu wa chuo cha VETA Mikumi kutumia mafunzo waliyoyapata kujitengenezea ajira binafsi badala ya kusubiri kuajiriwa.

Akizungumza katika mahafali ya 49 ya chuo hicho Mgoyi amesema, mafunzo ya ufundi stadi waliyoyapata vijana hao ni msingi wa ajira kwa dunia ya sasa yenye mabadiliko makubwa na ya kasi ya ukuaji wa teknolojia.

Alisema mafunzo ya ufundi stadi yemejikita zaidi kwenye vitendo na hivyo kumwezesha muhitimu kujiajiri kwa urahisi huku akiwapongeza wazazi kwa uamuzi sahihi walioufanya wa kuwapeleka vijana wao kusomea ufundi.

Aliwashauri vijana kuunda vikundi ili waweze kujiajiri kwa urahisi kwani mbinu hiyo huleta unafuu wa shughuli zao na kujipatia kipato kwa urahisi.

Mgoyi aliwataka wahitimu kuendeleza nidhamu waliyokuwa nayo wakati wapo chuoni kwenye shughuli wanazotarajia kufanya kwani kazi bila nidhamu haitakuwa na tija katika kuendeleza maisha yao na yale ya jamii zao.

Akimkaribisha mgeni rasmi katika hafla hiyo, Mkuu wa Chuo cha VETA Mikumi Christopher Ayo aliwahamasisha vijana kutumia fursa za mafunzo ya ufundi stadi zinazotolewa na VETA ili kujihakikishia ajira na kujiletea maendeleo yao binafsi na ya taifa.

Alisema katika muhula wa kuanzia Januari, 2016 chuo hicho kimesajili jumla ya wanafunzi 659 wa kozi ndefu kati yao wavulana 443 na wasichana 216 na kutoa mafunzo ya muda mfupi (miezi 3-6) kwa vijana 2,160 kati yao wavulana 1,174 na wasichana 986.

Ayo alitaja  ukosefu wa maji safi na salama kama moja ya changamoto inayokabili chuo hicho na mji wa Mikumi kwa ujumla na kwamba imekuwa kikwazo kikubwa cha maendeleo na maisha bora kwa wanajamii chuoni hapo na kumwomba Mkuu wa Wilaya kutafutia ufumbuzi wa suala hilo kwani ni la muda mrefu.
Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Adamu Mgoyi akitembelea maonesho ya fani mbalimbali zinazotolewa katika chuo cha VETA Mikumi katika Mahafali 49.
Wanafunzi wa kozi ya Utalii wakicheza ngoma za utamaduni katika mahafali ya 49, VETA yaliyofanyika katika Chuo cha VETA, Mikumi wilayani Kilosa mkoani Morogoro .
Mkuu wa Chuo cha VETA, Mikumi, Christopher Ayo akizungumza na wahitimu wa chuo hicho katika mahafali ya 49 .
Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Adamu Mgoyi akizungumza katika mahafali ya 49 ya Chuo cha VETA, Mikumi wilayani Kilosa mkoani Morogoro.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...