Wajasiriamali waliopo mkoani Kigoma wametakiwa kutumia raslimali mbalimbali zilizopo mkoani humo na fursa zinazojitokeza kwa sasa kuibua miradi ya biashara na kuendesha biashara yao kitaalamu wakiwa na malengo ya kujikwamua kutoka katika hali ya umaskini. Ushauri huo umetolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji , Yuda Thadeus Mboya, wakati wa ufunguzi wa mafunzo maalumu ya mbinu za kuendeleza wajasiriamali yaliyoandaliwa na taasisi ya Tanzania Private Sector Foundation (TPSF) na kufanyika katika ukumbi wa St.Martha mjini Kigoma. 

Alisema serikali imefungua milango ya kuwasaidia wafanyabiashara wadogo kwa kutumia fursa zilizopo hivyo aliwataka kushiriki mafunzo mbalimbali ya mbinu za biashara na kuibua miradi ya biashara na kuwa na utayari wa kukabiliana na changamoto mbalimbali zilizopo katika biashara kwa kipindi hiki mojawapo ikiwa ni ushindani mkubwa na kufanya biashara kwa kufuata njia halali zinazotakiwa ikiwemo kulipa kodi za serikali kwa mujibu wa sheria. 

Hivi sasa biashara zinafanyika katika mazingira ya ushindani na wateja wanahitaji bidhaa zenye ubora hivyo haitakiwi ubabaishaji wa aina yoyote kwa mfanyabiashara anayetaka mafanikio”.

Alisema Mboya. Aliipongeza taasisi ya TPSF kwa kuendesha miradi ya mafunzo kwa wajasiariamali sehemu mbalimbali nchini “Nawapongeza kwa kuwafikishia mafunzo wajasiriamali wa ngazi za chini katika ngazi ya mikoa na wilaya kwa kuwa wafanyabiashara wakipata mafunzo kama haya kwa vyovyote wataweza kupata mafanikio katika shughuli zao”.Alisema . 
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji Yuda Thadeus Mboya (katikati) akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina ya wajasiriamali iliyoandaliwa na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (Tanzania Private Sector Foundation),(Kulia) Meneja wa SIDO mkoa Kigoma, Gervas Ntahamba na (wa pili kushoto) Mwenyekiti wa chama cha Wafanyabiashara na wenye viwanda mkoa Kigoma (TCCIA), Ramadhani Gange. 
Mwenyekiti wa chama cha Wafanyabiashara na wenye viwanda mkoa Kigoma (TCCIA), Ramadhani Gange (wa pili kushoto aliyesimama) akitoa neno la shukrani kwa mgeni Rasmi wakati wa ufunguzi wa semina kwa wajasiliamali iliyotayarishwa na taasisi ya sekta binafasi Tanzania (TPSF) .

Baadhi ya wajasiliamali wa Manispaa ya Kigoma Ujiji wakijadiliana mada mbalimbali zilizotolewa na wawezeshaji wakati wa semina ya wajasiriamali iliyoandaliwa na taasisi ya sekta binafasi Tanzania (TPSF).


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...