THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

WAKAZI WA KIBAMBA WILAYANI UBUNGO WAZUIA MSAFARA MAKONDA WAKITAKA WASIKILIZWE KERO ZAO

Wakazi wa Kibamba Wilayani Ubungo wamezuia msafara wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda huku wakiwa wamebeba mabango yanayoonesha kero zao mbalimbali ikiwemo na kero ya kudhulimiwa maeneo yao ya.

Akizungumza na wakazi hao waliokuwa wamesimamisha msafara huo, Mkuu wa Wilaya hiyo Humphrey Polepole aliwataka wakazi hao kufuata utaratibu Kwani madai yao yamefika mezani kwake na baadhi yameanza kushughulikiwa kwa watu kulipwa fidia zao kutokana na kupisha eneo la chuo na hospitali ya MUHAS .

DC Polepole amesisitiza kuwa serikali ipo pamoja na wananchi hao ambao wengine wanadai fidia ya eneo la kwembe na Rais Mstaafu Jakaya Kikwete aliahidi kuwa watalipwa, vilevile Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliwahidi kuwa serikali itazifanyia kazi ahadi zote zilizoachwa na serikali iliyopita. 

DC Polepole ameongeza kuwa kwa wale wakazi waliopo maeneo ya hifadhi ya barabara serikali itaendelea na msimamo wake wa upanuzi wa barabara kama alivyohaidi Rais Magufuli jana kwenye Mkutano wa hadhara wa RC Makonda uliofanyika Maramba Mawili.

Kwa upande wake RC Makonda ambaye alishuka baada ya wakazi hao kuonekana kugoma kupisha msafara hu na kuwaambia kufuata utaratibu kutokana na majibu ya awali ya DC Polepole.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda akizungumza na wananchi wa Kibamba Wilayani Ubungo huku wakiwa wamebeba mabango yanayoonesha kuwa wamedhulumiwa ardhi yao.
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo,Humphrey Polepole akizungumza na wananchi wa Kibamba Wilayani Ubungo huku wakiwa wamebeba mabango yanayoonesha kero zao mbalimbali wanazotaka zipatiwe majibu
wananchi wa Kibamba Wilayani Ubungo wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda alipokuwa akizungumza nao kwenye ziara yake ya kusikiliza na kutatua kero za Wananchi.Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii