Akizungumza
wakati wa uwekaji jiwe la msingi katika kiwanda cha kutengeneza
vifungashio kilichopo wilayani Kihaba mkoani Pwani Katibu Mkuu Wizara ya
Viwanda, Biashara na Uwekezaji Dkt. Adelhelm Meru amesema kuwa tukiwa
tunaelekea katika nchi ya viwanda serikali inajukumu la kutoa
ushirikiano wa kutosha kwa wawekezaji nchini.Dkt. Adelhelm amesema kuwa
viongozi hao hawana budi kuiga mfano wa Mkuu wa Mkoa wa Pwani na Mkuu wa
Wilaya ya Kibaha kwa ushirikiano wanaoutoa kwa wawekezaji ikiwemo
kutenga maeneo kwa ajili ya ujenzi wa viwanda katika mkoa huo.
“Dhumuni
la serikali kwa sasa ni kuhakikisha tunaifikia nchi ya uchumi wa kati
kupitia viwanda,na hili tutalitekeleza pia kwa kushirikiana na sekta
binafsi na ni jukumu la viongozi ikiwemo wakuu wa wilaya na wakuu wa
mikoa nchini kote kutoa ushirikiano wa kutosha kwa wawekezaji ikiwemo
kutenga maeneo kwa ajili ya ujenzi wa viwanda”. Alisema Dkt. Adelhelm.
Dkt.
Adelhelm aliongeza kuwa mpaka ifikapo mwaka 2020 Serikali imepanga
kuhakikisha sekta ya viwanda nchini inachangia asilimia 15 kwenye pato
la taifa kutoka asilimia 7.3 iliyopo hivi sasa.Pia Dkt. Adelhelm alisema
kuwa Serikali imepanga kuongeza idadi ya ajira za viwandani na ajira
zitokanazo na sekta ya viwanda hadi kufikia asilimia 40 ifikapo mwaka
2020.
Naye
Mtendaji Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Taifa(NDC) Bw. Mlingi Mkucha
amesema kuwa shirika hilo litaendelea kutoa ushirikiano kwa wawekezaji
wote wenye nia ya kuwekeza katika viwanda ikiwemo kupitia maandiko ya
miradi yao na kuwasimamia ili kuhakikisha kwa pamoja wanatimiza lengo la
serikali ya awamu ya tano ya kufikia uchumi wa kati kupitia viwanda.
Bw.
Mkucha aliongeza kuwa katika wilaya ya Kibaha kuna hekari 330
zilizotengwa kwa ajili ya viwanda vya aina mbalimbali ikiwamo viwanda
vya kuunganisha magari, vuwanda vya madawa na viwanda vya nguo hivyo
kama kuna muwekezaji mwenye nia ya kuwekeza katika sekta hizo aende
katika ofisi za Shirika hilo ili kuweza kujadili namna ya kutekeleza
suala hilo.
Naye
Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Bi. Asumpta Mshana alisema kuwa ujenzi wa
kiwanda hicho katika mkoa wa pwani ni mwendelezo wa jitihada za kumuunga
mkono Rais Magufuli ya kufikia uchumi wa kati kupitia viwanda.Kwa
upande wake Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kiwanda cha kutengeneza
vifungashio cha Global Packaging Bw. Joseph Wasonga alishukuru jitihada
za serikali na taasisi zake kwa ushirikiano wanaoupata tangu wakiwa na
wazo la kuanzisha kiwanda hicho hadi kufikia hatua hiyo ya uzinduzi.
Bw.
Wasonga aliongeza kuwa dhumuni la kiwanda hicho ni kuzalisha
vifungashio milioni 16 hadi milioni 20 kwa mwaka na kuongeza zaidi idadi
ya ajira kwa wakazi wa maeneo yanayozunguka kiwanda hicho na maeneo ya
jirani.Kiwanda cha hicho kinamilikiwa kwa ubia kati ya Shirika la
Maendeleo la Taifa(NDC) na kampuni ya Wande Printing and Packaging
inayomilikiwa na mzawa.
Katibu
Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Dkt.Adelhelm Meru
akiongea wakati wa hafla ya uwekaji jiwe la msingi katika kiwanda cha
kutengeneza vifungashio cha Global Packaging Limited kilichopo Wilayani
Kibaha Mkoani Pwani ambapo alimpongeza muwekezaji wa kiwanda hicho na
kutoa rai kwa wakuu wa wilaya na mikoa nchini kuweka mazingira mazuri
kwa ajili ya wawekezaji ikiwemo kutenga maeneo maalum kwa ajili ya
viwanda kama ilivyo katika mkoa wa Pwani.
Katibu
Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Dkt.Adelhelm Meru
(katikati)akikata utepe kuashirika uwekaji wa jiwe la msingi katika
kiwanda cha kutengeneza vifungashio cha Global Packaging kilichopo
Wilayani Kibaha Mkoani Pwani, wakwanza kushoto ni Mkurugenzi Muendeshaji
wa Kiwanda hicho Bw. Joseph Wasonga, watatu kutoka kushoto ni Mtendaji
Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) Mlingi Mkucha akifuatiwa na
Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Bi. Asumpta Mshana.
Katibu
Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Dkt.Adelhelm Meru
(katikati mwenye miwani), Mtendaji Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Taifa
(NDC) Mlingi Mkucha (mwenye tai nyekundu), Mkurugenzi Muendeshaji wa
Kiwanda cha vifungashio Bw. Joseph Wasonga (wanne kutoka kulia) na Mkuu
wa Wilaya ya Kibaha Bi. Asumpta Mshana wakiwa katika picha ya pamoja na
wafanyakazi wa Kiwanda hicho na wafanyakazi wa NDC.PICHA HABARI NA
HASSAN SILAYO
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...