Mwenyekiti wa Mfuko wa Wanawake Tanzania, Profesa Ruth Meena (katikati) akisoma tamko la wanawake kwa wanahabari kuelezea tathini ya mwaka mmoja wa Serikali ya awamu ya tano mara baada ya kufunguliwa kwa mkutano huo. Wengine ni viongozi na wajumbe wa mkutano huo.
WANAWAKE
kupitia Mfuko wa Wanawake Tanzania wamekutaka katika mkutano na kutoa
tathimini ya mwaka mmoja wa Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na
Rais Dk. John Pombe Magufuli. Mkutano huo ulioshirikisha wanawake kutoka
mikoa mbalimbali umefanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mtandao wa
Jinsia Tanzania, TGNP Mabibo jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
katika mkutano huo, Mwenyekiti wa mfuko huo, Profesa Ruth Meena
aliipongeza Serikali ya Dk. Magufuli kwa mafanikio ilioanza kuonesha
katika ukusanyaji na usimamizi wa mapato pamoja na mapambano dhidi ya
vitendo vya rushwa huku akiiomba Serikali kutambua pia kwa vitendo
mchango wa wanawake katika ujenzi na maendeleo ya nchini.
Aliyekuwa mgombea nafasi ya urais wa Chama cha ACT – Wazalendo, Anna
Mghwira (kulia) ambye pia ni Mwenyekiti wa chama hicho taifa akichangia
mada katika mkutano wa wanawake ulioandaliwa na Mfuko wa Wanawake
Tanzania.
Baadhi ya washiriki katika mkutano huo wakijadiliana masuala anuai.
Mkutano huo ulioshirikisha wanawake kutoka mikoa mbalimbali umefanyika
katika Ukumbi wa Mikutano wa Mtandao wa Jinsia Tanzania, TGNP Mabibo
jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa WFT, Mary Rusimbi (kushoto) akichangia mada katika mkutano huo.
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...