SERIKALI imesema kuwa itaendelea na utaratibu wa kuwalipa wastaafu wanaohudumiwa na Wizara ya Fedha na Mipango, pensheni yao kila mwezi kwa mujibu wa sharia ya mafao ya wastaafu Na. 371 badala ya kuwalipa malipo hayo kila baada ya miezi mitatu

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. DOTTO JAMES amesema kuwa uamuzi huo umetolewa baada ya kupitia na kujadili mapendekezo ya baadhi ya wastaafu waliofika Makao Makao Makuu ya Wizara ya Fedha Jijini Da ers salaam mwezi uliopita wakitaka serikali irejeshe utaratibu wa kuwalipa kila baada ya miezi mitatu mitatu ili waweze kujikimu kimaisha.

James amesema kuwa Wizara imepokea maombi kutoka kwa baadhi ya wastaafu kutaka kulipwa kila baada ya kipindi hicho huku wengine wakitaka kulipwa kila mwezi hatua ambayo imeifanya Serikali kuamua kulifanyia kazi suala hilo kwa kina na kuahidi kulitolea uamuzi hapo baadae.


Benny Mwaipaja, Msemaji Wizara ya Fedhana Mipango

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Hawa Wastaafu hata akili zao zimestaafu. Pesheni duniani kote inalipwa kila mwezi. Kama huwezi kutunza wewe mwenyewe unadhani Serikali kukulipa kila miezi mitatu ndio una save? Si uende Benki Mara moja kila baada ya miezi mitatu ama hata baada ya mwaka utazikuta fedha zako? Ya nini kuwasumbua wanaotaka kulipwa kila mwezi. Hivi kweli viongozi wa Serikali wanao muda wa kushughulika na watu kama hawa?

    ReplyDelete
  2. hii ni sawa ila kuna wastaafu mpaka wafike bank zipo mbali kiukweli wangeangalia wanaoweza kupewa mwezi wapewe

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...