Watalaam 25 wa afya kutoka nchi tisa za Afrika leo wametunukiwa vyeti vya kuhitimu mafunzo ya kupima masikio na kufundisha kuongea kwa watu wenye matatizo ya usikivu.

Mafunzo hayo yamewezeshwa na Kampuni ya MEDAL ya nchini Australia na kuhusisha washiriki kutoka nchi za Rwanda, Uganda ,Kenya , Zambia , Zimbabwe, Nigeria , Ghana, Malawi na Tanzania . Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ni mwenyeji wa mafunzo hayo.

Akikabidhi vyeti hivyo Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru ameishukuru Kampuni ya MEDAL kwa kuwezesha kutolewa kwa mafunzo hayo ambayo yanaisaidia Hospitali kupiga hatua katika mipango yake hususani katika suala la kutoa huduma kwa wale wenye matatizo ya usikivu.

Awali, Meneja wa Maendeleo Kanda ya Afrika Mohamed El Disouky amesema MEDEL wataendelea kushirikiana na wataalam mbalimbali wakiwemo wa Muhimbili ili kuhakikisha wanapata ujuzi wa kutosha katika kutoa huduma hiyo.

Mafunzo hayo yalianza Oktoba 29 mwaka huu jijini Dar es salaam na kumalizika Novemba 5, mwaka huu.
Mkurugenzi Mtendaji, Profesa Museru akikabidhi cheti kwa mmoja wa washiriki kutoka Muhimbili, JohnBosco Kambanga.
Mshiriki kutoka Rwanda, Fidel Munezero akipongezwa baada ya kukabidhiwa cheti Leo.
 
Wadau wa Afya wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumalizika kwa mafunzo ya kupima masikio na kuongea yalioanza Oktoba 29, mwaka huu na kufungwa leo Novemba 5, 2016 jijini Dar es Salaam.Picha na John Stephen, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...