Na Humphrey Shao,Globu ya Jamii

Watanzania wametakiwa kujiingiza katika kilimo cha misitu ya kupandwa ili waweze kujikwamua kiuchumi na kuomngeza ajira kwa vijana .

Kauli hiyo imesemwa  leo na Waziri wa Maliasili na utalii ,Profesa Jumanne Maghembe, alipokuwa akifungua mkutano wa wawekezaji wa misitu ya kupandwa ulioandaliwa na tasisi ya Uongozi Institute kwa kushirikiana na serikali ya Finland.

“Mpango uliopo sasa ni kuakikisha kuwa kila mtu anafaidika na mti kuanzia atua ya awali hadi pale wakati wa kuvuna kwani mtu atalipwa fedha kwa namna gani miti yake inavyokuwa na kunyonya hewa ya ukaa inayodhalishwa viwandani hivyo hakuna mtu atakaye acha kupanda miti” Amesema Maghembe.

Amesema kuwa kwa mujibu wa ripoti iliyotoka mwaka 2014 inasema kuwa Tanzania imeweza kutunza jumla ya ekari 17 Milioni ambazo ni sawa na asilimia 35% ya ardhi yote ambayo ipo hapa nchini .

Amesema kwa sasa asilimia 85% ya malighafi inayosambazwa katika viwanda mbalimbali nchini inatotokana na misitu ambayo inasimamiwa na Wakala wa Misitu wa serikali(TFSA) .
Waziri wa Maliasili na Utalii,Profesa Jumanne Maghembe, akizungumza katika mkutano huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...