Na Genofeva Matemu – WHUSM
Wazalishaji wa kazi za filamu nchini wametakiwa kuzalisha kazi zenye ubora na
viwango vinavyotakiwa ili Tanzania iweze kupambana na mataifa mengine katika
sekta ya filamu.
Rai hiyo imetolewa na Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo wakati wa
ziara iliyofanywa na Bodi ya Filamu pamoja na makampuni mbalimbali ya
watayarishaji Jana Jijini Dar es Salaam katika Studio ya Wanene Entertainment.
“Ili kuleta maendeleo chana ndani ya Sekta ya Filamu hatuna budi kuwa mabalozi wa
tasnia hii kwa kuboresha ubora wa filamu zetu na kuweza kuliteka soko la ndani na
nje ya nchi” alisema Bibi. Fissoo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya Wanene Entartainment Bw. Darsh
Pandit amesema kuwa kampuni ya Wanene imekubali kushirikiana na watayarishaji
wa filamu za ndani ili kutoa filamu zenye ubora ambazo zitaleta mapinduzi kwenye
tasnia ya filamu nchini.
Kwa upande wao watayarishaji wa ndani wa kazi za filamu wameliomba Baraza la
Kiswahili la Taifa (BAKITA) kuanzisha kitengo maalum cha kutafsiri filamu za
kitanzania ili ziwe na tafsiri inayoendana na kazi husika.
Wazalishaji wa filamu kutoka makampuni mbalimbali hapa nchini wametembelea
studio hiyo ili kuweza kuangalia uwezekano wa kushirikiana katika kuzalisha filamu
zenye ubora kupanua wigo wa tasnia ya filamu hapa nchini.
Baadhi ya Watayarishaji waliofanya ziara hiyo katika Studio za Wanene Entertainment
ni pamoja na kampuni za Inspiration Image, Cut2cut Entertainment, 5 Effects, Steps
na UWAFIMU.
Watayarishaji wa filamu kutoka makampuni mbalimbali wakiangalia moja ya
kifaa kinachotumika kuandaa filamu katika Studio za Wanene Entertainment
walipotembelea studio hizo katika kuboresha ubora wa filamu nchini Jana Jijini Dar es
Salaam. Kushoto waliokaa ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo.
Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo akijaribu kupiga ngoma
zinazotumika kuandaa kazi za muziki na filamu katika Studio ya Wanene
Entertainment wakati wa ziara iliyofanywa na watayarishaji wa kazi za filamu
kuboresha ubora wa filamu nchini Jana Jijini Dar es Salaam.
Watayarishaji wa filamu kutoka makampuni mbalimbali wakiangalia moja ya
chumba kinachotumika kuandaa filamu katika Studio za Wanene Entertainment
walipotembelea studio hizo katika kuboresha ubora wa filamu nchini Jana Jijini Dar es
Salaam. Kulia ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo.
Watayarishaji wa filamu kutoka makampuni mbalimbali, watendaji kutoka Bodi
ya Filamu pamoja na watayarishaji kutoka Studio ya Wanene Entertainment katika
picha ya pamoja wakati wa ziara iliyofanywa na watayarishaji hao katika Studio za
Wanene Entertainment kuboresha ubora wa filamu nchini Jana Jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...