Na Amina Kibwana, Globu ya Jamii

Jeshi la Polisi Mkoa wa Dar es Salaam, linawashikilia watu watato wanaotuhumiwa kuwa ni majambazi baada ya kupatikana na mali ya wizi ambayo inadaiwa kuwa iliibiwa nyumbani kwa Patriki Samari maeneo ya Tuangoma mtaa wa Msaki Mbagala jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda maalum ya Dar es salaam, Kamishna Simon Sirro amesema kuwa watu hao wanadaiwa kuvunja mlango na kuiba vitu mbalimbali  ikiwa ni pamoja na kiasi cha fedha cha shilingi Milioni kumi na laki moja na themanini elfu ,Televisheni nne aina ya Samsung, Laptop mbili aina ya hp, simu mbili aina ya samsung, External hard drive moja, deck, pamoja na King'amuzi.

Aidha Kamanda Sirro alitaja majina ya watuhumiwa hao kuwa ni pamoja na Penza Selemani, Mwarami Nasoto, Salum Taidini, Sweed Shaaban (40) mkazi wa kinondoni manyanya na Mussa Ismail (47), mkazi wa Sinza ambaye ni dereva.

Sirro ameongeza kuwa sambamba na tukio hilo pia Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limefanikiwa kukamata wanawake wanne na watoto wanne waliokuwa wamefichwa kwenye kambi ndani ya msitu, katika eneo la Kilongoni Vikindu wakiwa wamekusanywa kwenye nyumba moja kwa lengo la kufundishwa mambo ya harakati za kigaidi.

Amesema watoto hao ni Fatuma Shaabani (2), Abdulrahmani Shaabani (8) na Asha Shaaban (8) ambao ni wanafunzi wa darasa la nne katika shule ya msingi Jitihada Kitunda na Aisha Shaabani (13) mwanafunzi wa darasa la saba katika shule ya msingi Kizenge Kitunda, ambao walitoroshwa na mama yao Salma Mohammed ambaye ameingizwa katika harakati za kigaidi.

Jeshi la polisi linaendelea kuwashikilia wanawake hao pamoja na watoto kwa ajili ya kuendelea na mahojiano ili kuweza kubaini mtandao mzima katika suala hilo na kutokomeza tabia hii ya kuwaachisha watoto wadogo shule na kuwaingiza katika vitendo vya uhalifu.

Katika tukio lingine Kikosi cha Polisi kanda Maalum cha kuzuia wizi kimefanikiwa kukamata gari aina ya toyota land cruiser lanye namba za usajiri T616 DCH ambayo ni mali ya Joseph Kayawaya iliyiripotiwa kuibiwa jijini Dar es Salaam.

Jeshi la polisi linaendelea kumshikilia mtuhumiwa Demestrious Apolonary ambaye ni Padri wa kanisa katoliki Sumbawanga kwa ajili ya mahojiano,na upelelezi utakapokamilika  mtuhumiwa huyo atapelekwa mahakamani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...