WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametoa siku 18 kwa Mkandarasi wa umeme kwenye kiwanda cha Kiluwa Steel Group awe amemaliza kazi ya kuweka ume mkubwa ili kiwanda hicho kianze kazi.

Ametoa agizo hilo leo (Jumamosi, Novemba 19, 2016) wakati akizungumza na wananchi na viongozi mbalimbali wa Serikali na wa Mkoa wa Pwani waliofika kiwandani hapo eneo la Mlandizi wakati akikagua utekelezaji wa maagizo aliyoyatoa Julai 12, mwaka huu alipozuru kiwanda kwa mara ya kwanza.

“Nilipokuwa hapa mara ya kwanza niliagiza itengenezwe njia ya reli kutoka njia panda ya reli ya kati, lakini pia niliagiwa uwekwe umeme wa msongo mkubwa ili kiwanda kiweze kuanza uzalishaji mapema mwakani. Nimefarijika kukuta maagizo haya yametekelezwa kwa kiasi kikubwa isipokuwa hili la umeme,” amesema.

“Mkandarasi ameomba siku 14, nimempa hadi tarehe 7 Desemba ahakikishe umeme unafanya kazi kwa kiwango kinachotakiwa. Sasa hivi wameanza test lakini muda ili transforma iweze kuhimili mzigo mkubwa… hili ni suala la kitaalamu kwa hiyo tuwape muda.”

Waziri Mkuu pia amesema amefarijika kusikia kwa orodha ya watu wanaodai fidia sababu ya kuoisha njia ya reli ijengwe, imeshawasilishwa kwa Mkuu wa Mkoa na mwenye kiwanda yuko tayari kuwalipa maa taratibu zitakapokamilika.

Mapema, akiwasilisha taarifa fupi, Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Eng. Evarist Ndikilo alisema haelewi ni kwa nini mkandarasi huyo anazidi kuomba siku 14 ili kukamilisha wakati aliahidi kuwa 14 za awali zingetosha kukamilisha kazi hiyo.

Kuhusu fidia kwa wananchi na Halmashauri ya Wilaya hiyo, Mkuu huyo wa Mkoa alisema wananchi waliopisha njia wanadai fidia ya sh. milioni 95.76 na Halmashauri inadai sh. milioni 307.26 na kwamba jumla yote inafikia sh. milioni 403.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...