WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameliegiza Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha lifanye maamuzi ya kupima ardhi haraka na kutenga maeneo kwa ajili makazi na viwanda ili kujiandaa na uwekezaji mkubwa.

Ametoa agizo hilo leo mchana (Jumamosi, Novemba 19, 2016) wakati akizungumza na wananchi na viongozi mbalimbali wa Serikali na wa Mkoa wa Pwani mara baada ya kukagua kiwanda cha kutengeneza magari ya zimamoto na matrekta cha Equator SUMA JKT Limited kilichopo Ruvu JKT, wilayani Kibaha mkoani Pwani.  

“Jiji la Dar es Salaam limejaa, na Kibaha mjini pia hawana ardhi ya kutosha kwa kimbilio pekee hivi sasa ni Kibaha Vijijini. Baraza la Madiwani fanyeni maamuzi, pimeni ardhi na mtenge maeneo ya makazi, viwanda na taasisi za elimu ili mkipata wawekezaji iwe rahisi kuwapa maeneo,” amesema.

Waziri Mkuu amesema ujenzi wa kiwanda hicho utakuwa mkombozi kwa taasisi nyingi na halmashauri nyingi nchini kwani zilikuwa zinashindwa kumudu bei ya kununua magari ya zimamoto. “Baadhi ya Halmashauri nyingi zilikuwa zinanunua gari moja kwa sh. milioni 500 na hiki ni kiasi kikubwa mno kwa hiyo kiwanda hiki kitakuwa mkombozi kwa taasisi nyingi na halmashauri zetu,” amesema.

Amesema maeneo mengi nchini yanahitaji magari ya zimamoto lakini yalikuwa yanashndwa kumudu bei za magari hayo. Aliyataja maeneo hayo kuwa ni viwanja vya ndege, bandari, taasisi zilizo chini ya TAMISEMI kama vile shule za sekondari za bweni, Majiji, miji mikuu, Manispaa na Halmashauri za Wilaya.

Amesema ameguswa kukuta kiwanda hicho pia kina uwezo wa kutengeneza matreka na zana za kilimo (farm implements) kwani asilimia kubwa ya Watanzania ni wakulima na wanategemea jembe la mkono. “Kupitia kiwanda hiki, matrekta mengi yataunganishwa na nina imani bei itakuwa ya chini ili wananchi waweze kumudu.”
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli nchini TRL, Masanja Kadogosa (kulia) kuhusu ujenzi  wa reli  inayounganisha  reli ya kati na  kiwanda cha Kiluwa Still Group cha Mlandizi Pwani Novemba 19, 2016  . Kulia kwake ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa. 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua mitambo ya kiwanda cha chuma cha Kiluwa Still Group kilichopo Mlandizi Pwani Novemba 19,2016 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
 Waziri Mkuu, Kassim  Majaliwa akizungumza baada ya kukagua  maendeleo ya ujenzi wa kiwanda cha Kiluwa Still Group cha Mlandizi mkoani Pwani  Novemba 19, 2016.  Kushoto ni  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa 
 Waziri  Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua kianda cha kuunganisha magari ya zimamoto na matrekta cha Equator SUMMA kilichopo Mlandizi mkoani Pwani Novemba 19,2016(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...