Na Veronica Simba.

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amekutana na Ujumbe kutoka Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japani (JICA) na kufanya mazungumzo kuhusu maendeleo ya miradi mbalimbali ya sekta ya nishati nchini inayofadhiliwa na shirika hilo.

Kikao hicho kilifanyika Novemba 17 mwaka huu katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara na kuhudhuriwa na viongozi waandamizi kutoka sekta ya nishati ambao ni pamoja na Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Sekta ya Nishati, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo, Kaimu Kamishna wa Nishati na Masuala ya Petroli - James Andilile, Kaimu Kamishna Msaidizi wa Nishati Sehemu ya Petroli – Mwanamani Kidaya na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Mhandisi Kapuulya Musomba.
Ujumbe wa JICA uliongozwa na Mwakilishi wake Mkuu hapa nchini, Toshio Nagase.
 Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto), akisisitiza jambo katika kikao baina yake na Ujumbe kutoka JICA. Kushoto kwake ni Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Nishati - Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo, Kaimu Kamishna wa Nishati na Maendeleo ya Petroli - James Andilile, Kaimu Kamishna Msaidizi wa Nishati Sehemu ya Petroli – Mwanamani Kidaya na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Mhandisi Kapuulya Musomba. 
 Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (Kulia), akiwasikiliza baadhi ya Maofisa kutoka JICA, wakati wakisaini Kitabu cha Wageni ofisini kwake baada ya kikao baina yao kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hivi karibuni.
 Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe kutoka JICA, walipomtembelea ofisini kwake hivi karibuni na kufanya mazungumzo kuhusu maendeleo ya miradi mbalimbali ya Sekta ya Nishati inayofadhiliwa na Shirika hilo hapa nchini.
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Digital Grid kutoka Japan, inayojishughulisha na usambazaji wa vifaa vya umeme wa jua hapa nchini, Bwana Akita (kulia), akielezea kuhusu utendaji kazi wa kampuni yake kwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, watendaji mbalimbali wa Wizara na Taasisi zilizo chini ya Wizara pamoja na Ujumbe kutoka JICA.
Kaimu Kamishna wa Nishati na Masuala ya Petroli, James Andilile (mwenye tai nyekundu-kulia), akifafanua jambo kwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, wakati wa kikao baina ya Waziri na Ujumbe kutoka JICA. Kulia kwa Waziri ni Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Sekta ya Nishati, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...