Na Rhoda James.
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo amekutana na
Waziri wa Migodi na Nishati wa Namibia, Obeth Kandjoze na
kuzungumza masuala mbalimbali kuhusu sekta wanazozisimamia.
Kikao hicho kilichofanyika katika Ukumbi wa Wizara ya Nishati na Madini
kilihudhuriwa na Viongozi Waandamizi Kutoka Wizara ya Nishati na
Madini, Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Shirika la
Umeme Tanzania (TANESCO), Wakala wa Nishati Vijijini (REA),
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) na
Meneja Mkuu wa Kampuni ya Maurel et Prom Tanzania na Namibia,
Christophe Maitre pamoja na Ujumbe kutoka Wizara ya Migodi na
Nishati.
Profesa Muhongo alielezea kuhusu, ugunduzi wa gesi asilia ambao
umefikia futi za ujazo wa trilioni 57.25T. Ujenzi wa mabomba ya
kusafirishia gesi asilia kama vile Mradi wa Songo Songo, Mnazi Bay na
ule wa kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam.
Aliongeza kuwa, Serikali ya Tanzania inatekeleza miradi mikubwa ikiwa
ni pamoja na Mradi wa Gesi Asilia kimiminika (Liquefied Natural Gesi)
unaotarajiwa kujengwa mkoani Lindi, Kiwanda cha kutengeneza mbolea
na ujenzi wa Bomba la Mafuta kutoka Hoima Uganda hadi Bandari ya
Tanga Tanzania.
Pia, alizungumzia kuhusu madini, akisema kuwa Tanzania imebarikiwa
kuwa na Madini mengi ikiwa ni pamoja na Uranium ambapo alimuomba
Waziri Kandjoze wa Namibia kuangalia uwezekano wa wataalam wa
Tanzania kwenda kujifunza zaidi kuhusu madini hayo nchini Namibia
kwani nchi hiyo imepiga hatua katika masuala ya uchimbaji wa madini
husika.
Kwa upande wake, Waziri Kandjoze aliishukuru Serikali ya Tanzania
kwa mapokezi mazuri na kusema kuwa, Namibia ina uzoefu mkubwa
katika masula ya uchimbaji madini ya Uranium. Namibia ni nchi ya tano
duniani katika uzalishaji wa Uranium ambapo madini hayo yanauzwa nje
ya nchi na kuzalishia umeme.
Waziri Kandjoze alisema kuwa, atatembelea Taasisi zilizopo chini ya
Wizara ikiwa ni pamoja na TPDC, TANESCO na EWURA ili kupata
elimu zaidi kuhusu sekta za Nishati na Madini.
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kushoto)
akielezea uzoefu wa Tanzania katika masuala ya Sekta za Nishati na
Madini. Kulia kwake ni Waziri wa Migodi na Nishati wa Namibia, Obeth
Kandjoze. Wengine katika picha ni viongozi waandamizi kutoka Wizara
ya Nishati na Madini na Taasisi zake pamoja na Ujumbe kutoka Wizara
ya Migodi na Nishati ya Namibia.
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kulia)
akimsikiliza mtaalam kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati
na Maji (EWURA) (hayupo pichani) akielezea kuhusu tozo mbalimbali
ikiwemo ile ya tariff. Kulia kwake ni Waziri wa Migodi na Nishati wa
Namibia, Obeth Kandjoze. Wengine katika picha ni Ujumbe kutoka
Namibia.
Waziri wa Migodi na Nishati wa Namibia, Obeth Kandjoze (akisaini
kitabu cha wageni) ofisini kwake. Waziri wa Nishati na Madini, Profesa
Sospeter Muhongo(anayeshuhudia).
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (wa pili kulia)
akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Migodi na Nishati wa
Namibia, Obeth Kandjoze pamoja na Ujumbe kutoka Namibia.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...