Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Dkt Harrison Mwakyembe amekutana na mwakilishi wa Taasisi Isiyo ya Kiserikali ya Kupitia Hali ya Haki za Binadamu kanda ya Afrika Bw, Gilbert Onyango na kuzungumza jinsi ya kusaidia utekelezaji wa mapendekezo 130 ambayo Serikali iliyakubali mbele ya Baraza la Haki za Binadamu wakati wa kupitia Ripoti ya Tathmini ya Hali ya Haki za Binadamu
.Mhe. Waziri Mwakyembe amesema Serikali kama ambavyo ilivyoridhia mapendekezo hayo itasimama imara kuhakikisha yanatekelezwa kikamilifu na hivyo kuimarisha hali ya haki za binadamu nchini.

Amesema nia ya Serikali ni kuona haki za bindamu nchini zinaheshimiwa bila ya kuingilia au kukiuka mila, tamaduni , desturi na imani za kidini ambazo Tanzania imekuwa ikizifuata au kuziamini tangu enzi.

Nae bw. Onyango alisema kwamba wao kama taasisi isiyo ya kiserikali wanafanya kazi na serikali mbalimbali duniani, taasisi zisizo za serikali na Umoja wa Mataifa katika kuhakikisha haki za binadamu zinaimarishwa na kuthaminiwa na kuongeza kuwa lengo hasa la kukutana kwake ni kujitambulisha na kuomba kufanya kazi na serikali katika kuhakikisha mapendekezo yaliyokubaliwa yanatekelezwa kikamailifu.

Pia aliomba kupatiwa nafasi ya kutoa mafunzo jinsi ya utekelezaji huo kwa taasisi na watumishi wa umma wanaohusika na utekelezaji wa mapendekezo hayo ili kufanikisha mpango wa utekelezaji wa mapendekezo hayo.

Alisema kwamba lengo lao kuu ni kuunganisha mpango wa tathmini ya hali ya haki za binadamu nchini ili uendane na mpango wa malengo ya milenia ili kuweza kufikia maendeleo ya kweli huku haki za binadamu zikiimarishwa na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa.

Mwezi Septemba 2016, Serikali iliyakataa mapendekezo 94, kuyaangalia upya mapendekezo 25 na kukubali 130 kati ya 227 yaliyotolewa na mataifa wanachama wa Umoja wa Mataifa, likiwemo suala la hali ya kisiasa Zanzibar. Tamko hilo lilitolewa kwenye mkutano wa Baraza la Haki za Binadamu wakati wa kupitisha Ripoti ya Tathmini ya Dunia (UPR) mbele ya Baraza la Haki za Binadamu wakati wa kupitia Ripoti ya Tathmini ya Hali ya Haki za Binadamu kwa nchi wanachama uliofanyika mjini Geneva nchini 

Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Dkt Harrison Mwakyembe (katikati) akiongea na mwakilishi wa Taasisi Isiyo ya Kiserikali ya Kupitia Hali ya Haki za Binadamu kanda ya Afrika Bw, Gilbert Onyango (kulia) alipomtembelea leo (16/11/2016) ofisini kwake jijini Dar Es Salaam. Wengine pichani ni Mkurugenzi wa Idara ya Katiba na Ufuatiliaji haki Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria Bw. Patience Ntwina (kushoto) na Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Katiba Bw. Stanley Kamana.

Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Dkt Harrison Mwakyembe (kushoto) akiongea na mwakilishi wa Taasisi Isiyo ya Kiserikali ya Kupitia Hali ya Haki za Binadamu kanda ya Afrika Bw, Gilbert Onyango alipomtembelea leo (16/11/2016) ofisini kwake jijini Dar Es Salaam.

Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Dkt Harrison Mwakyembe (kushoto) akiongea na mwakilishi wa Taasisi Isiyo ya Kiserikali ya Kupitia Hali ya Haki za Binadamu kanda ya Afrika Bw, Gilbert Onyango alipomtembelea leo (16/11/2016) ofisini kwake jijini Dar Es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...