Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mwigulu Nchemba akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kumaliza kikao chake na Menejimenti ya Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) wakati alipofanya ziara ya kikazi Makao Makuu ya NIDA, Kinondoni, jijini Dar es Salaam leo. Mwigulu aliwaambia waandishi wa habari kuwa, NIDA itaanza kutoa namba za utambulisho kwa wananchi wote kuanzia mwezi Desemba mwaka huu, ambao wamesajiliwa kupitia mpango wa usajili wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC). Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Andrew Massawe.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Andrew Massawe (watano kushoto) akimuelezea jambo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (katikati) wakati Waziri huyo alipotembelea Makao Makuu ya Mamlaka hiyo, Kinondoni, jijini Dar es Salaam leo. Kiongozi huyo wa NIDA katika hotuba yake fupi kwa Waziri Mwigulu, alisema kuwa, NIDA itaanza kutoa namba za utambulisho kwa wananchi wote kuanzia mwezi Desemba mwaka huu, ambao wananchi hao wamesajiliwa kupitia mpango wa usajili wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (kushoto) akimsikiliza Kaimu Mkurugenzi wa Mifumo ya Kompyuta (TEHAMA) wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Mohamed Khamis (wapili kushoto) alipokuwa akielezea jinsi wanavyosajili taarifa mbalimbali za waombaji wa vitambulisho. Waziri Mwigulu alitembelea Kituo hicho cha Usajili na kujifunza kazi mbalimbali zinazofanywa na NIDA, jijini Dar es Salaam leo. Watatu kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Andrew Massawe.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Andrew Massawe (wapili kushoto-mbele) akimsindikiza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (kushoto mstari wa mbele) mara baada ya Waziri huyo kumaliza ziara yake ya kutembelea ofisi za NIDA Makao Makuu na ofisi zake za usajili wa taarifa mbalimbali za waombaji wa vitambulisho, zilizopo jijini Dar es Salaam. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...