Waziri wa Afya katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Tamasha la Kimataifa la Filamu Zanzibar ZIFF, Mhe.Mahmood Thabith Kombo, akizungumza kwenye Uzinduzi wa Tamasha la Uoneshaji wa Filamu kwa njia ya Sinema mkoani Geita, kwa niaba ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe.Nape Nhauye.

Uzinduzi huo ulifanyika jana katika Ukumbi wa Desire Park Geita ambapo Taasisi ya Sanaa Na Mazingira ya Kijani Consult Tanzania imeanzisha kampeni ya kuonesha bure Filamu mbalimbali kwa ajili ya kufikisha elimu kwa umma ikiwemo elimu ya Utunzaji wa Mazingira (Mabadiliko ya Tabianchi), Ufugaji wa kuku wa kienyeji, Usalama barabarani, Madawa ya kulevya, Madhara ya ndoa za utotoni miongoni mwa mambo mengi ya kijamii. Mradi huo umefadhiriwa na ZIFF.

Kutokana na Mwitikio wa wanatasnia ya Filamu mkoani Geita kuonesha shauku ya kuwa na Maonesho hayo ya Filamu, Mhe.Kombo alisema mwakani Tamasha la Kimataifa Zanzibar pia litafanyika mkoani Geita ikiwa ni sehemu ya ZIFF ni sehemu ya kusherehekea miaka 20 tangu kuanzishwa ZIFF.
Na BMG
Mhe.Kombo alisema mwakani Tamasha la Kimataifa Zanzibar pia litafanyika mkoani Geita ikiwa ni sehemu ya ZIFF ni sehemu ya kusherehekea miaka 20 tangu kuanzishwa ZIFF.
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Bi.Joyce Fessoo, akizungumza kwa niaba ya Serikali kwenye uzinduzi huo ambapo aliwahakikishia Wanatasnia ya Filamu mkoani Geita na nchini kwa ujumla kwamba Serikali itahakikisha inaboresha zaidi sanaa ya filamu ikiwemo kuendelea kutoa mafunzo ya filamu kwa wanatasnia hiyo ili filamu zinazozalishwa ziwe na ubora.

Aidha alidokeza kwamba Serikali inatoa baraka zote kuhusiana na Tamasha la Kimataifa la Filamu Zanzibar, pia kufanyika mkoani Geita hapo mwakani.
Mkuu wa Mkoa wa Geita, Meja Jenerali Mstaafu, Ezekiel Kyunga, akizungumza kwenye Uzinduzi wa Uoneshaji wa Filamu mkoani Geita, ambapo alisisitiza kwamba sanaa ni ajira hivyo wanatasnia hiyo watumie fursa mbalimbali ikiwemo mafunzo yanayotolewa na serikali ili kuboresha zaidi kazi zao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...