Itakumbukwa kwamba nyasi bandia kwa ajili ya uwanja huu zilikwama bandarini kwa muda mrefu baada ya TFF kutakiwa kulipiwa kodi ya zaidi ya shilingi Milioni 32 hali ambayo ilisababisha utekelezaji wake kusuasua.
Waziri Nape Nhauye amesema Serikali itaendelea kuboresha viwanja mbalimbali nchini ikiwemo kushirikiana na makampuni mbalimbali ili kukarabati viwanja vilivyopo ili Tanzania iwe sehemu bora hata kwa mataifa mengine kufika kwa ajili ya mazoezi na michezo mbalimbali hususani ya mpira wa miguu.
Altaf Hiran Mansoor ambaye ni mdau wa michezo Jijini Mwanza na Mkurugenzi wa Kampuni ya Mafuta ya MOIL, amesema kampuni hiyo iko tayari kuchangia ukarabati wa uwanja huo ikiwemo ujenzi wa majukwaa.
Uwanja mkongwe wa Nyamagana sasa unang'aa kwa viwango vingine, ambapo Waziri Nape amesema anashawishika kuandaa mechi ya kirafiki kati ya timu za Simba na Yanga zinazoundwa na wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, itakayochezewa kwenye uwanja huo.
Itakumbukwa kwamba Mwaka 1974 timu za Simba na Yanga zilikutana kwenye uwanja wa Nyamagana, kwenye Fainali ya Ligi ya Taifa ya Soka ambapo Yanga iliichapa Simba bao 2-1.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...