Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

KLABU ya soka ya Dar es Salaam Young Africa (Yanga) imeongoza kwa kuingiza fedha nyingi kwa kupitia mapato ya mlangoni tangu kuanza kutumika kwa mfumo wa tiketi za kielectronic.

Hayo yamesemwa leo na Meneja Masoko wa Selcom nchini, Juma Mgori alipokuwa katika mahojiano maalum na Globu ya jamii jijini Dar es Salaam.

Mgori amesema kuwa licha ya kuwepo kwa changamoto ya uelewa wa kutumia kadi hizo kwa mashabiki mpaka sasa Yanga ndio klabu inayoongoza kuingiza fedha nyingi ikifuatiwa na klabu ya Simba.

“mfumo huu umeweza kuzinufaisha sana timu hizi kwa namna moja au nyingine kwani zimeweza kuingiza fedha moja kwa moja kwenye akaunti zao bila ya kuwepo na utata wowote huku timu kama Toto Afrika ya Mwanza ikiwa imenufaika maradufu kwa kupata kiasi cha shilingi milioni tisa katika mechi moja tofauti na mechi za nyuma kabla ya mfumo wa electroniki ulivyoanza kutumika” amesema Mgori.

Mgori ameongeza kuwa ni muda sasa wa shirikisho la soko nchini TFF na Vilabu vya soka nchini kuanza kutoa elimu ya kutosha juu ya matumizi ya kadi hizo hili waweze kujiongezea kipato katika michezo mbalimbali itakayochezwa nchini.

Amesema wapo viongozi wakubwa tu wa vilabu vya soka hapa nchini ambao wamewapigia simu kwa jinsi gani walivyoweza kunufaika na mpango huu wa tiketi za electroniki.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...