Ongezeko la shughuli za kibindamu na viwanda kwa ujumla imesababisha kuongezeka kwa hewa ya ukaa na majanga yatokanayo na mabadiliko ya tabia nchi mfano mafuriko na joto kali ambalo husababisha magonjwa na athari kwa viumbe hai na binadamu kwa ujumla hasa katika miji mikubwa ikiwemo jiji la Dar es salaam. 
Katika kutekeleza na kuunga mkono kampeni ya utunzaji wa mazingira maarufu  kama “mti wangu” iliyozinduliwa na mkuu wa mkoa wa Dar es saalam , Mh Paul Makonda, kampuni ya simu za mkononi ya Airtel  kwa kushirikiana na wafanyakazi wake leo imeshiriki katika kupanda majani , miti na kuweka mbolea ili kutunza mazingira na kuyaweka katika hali ya kuvutia 
Bustani hiyo inayoanzia katika mataa ya Moroco hadi maeneo ya mgahawa wa Best Bite  katika barabara ya Ali Hassan Mwinyi ilikabidhiwa kwa kampuni ya Airtel na mh. Mkuu wa Mkoa kwa lengo la kuboresha na kutunza mazingira ya jiji la Dar es saalam  
Ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa kampeni hii, leo wafanyakazi wa Airtel kwa kushirikiana na serikali tunashirikia katika zoezi la kupanda majani na miti katika eneo la katikati ya barabara. Airtel tunaamini ili tuweze kufanya biashara tunahitaji mazingira bora na kwa kupitia kampeni hii ya mti wangu tunaunga mkono juhudi hizo kwa kuyatunza mazingira  yanayotuzunguka na kuyaweka katika hali ya usafi na kuvutia” alisema Airtel Afisa Mazinga wa Airtel ,Bwana Ncheye Mazoya  
Kwa upande wake Afisa Mazingira wa wilaya ya Kinondoni, Bwn Awadhi Kinajambo alisema “tunatoa shukurani kwa kampuni ya Airtel kwa kuunga mkono jitihada hizi za kutunza mazingira kupitia kampeni hii mahususi ya “Mti Wangu”. Tunaanmini juhudi hizi zitasaidia katika kuboresha hali hewa,kuondoa tishio la majanga yatokanayo na mabadiliko ya tabia nchi pamoja na kupendezsha jiji letu la Dar es salaam”. 
Natoa  wito kwa wakazi na wafanyabiashara wa maeneo haya kutokatiza kwenye bustani hii wala kutupa taka ili tuweze kuunga mkono kwa vitengo zoezi hili kuwa la mafanikio na kwa pamoja kutunza mazingara yetu. 
Afisa Mazingira wa Airtel, Ncheye Mazoya akimwagilia mti baada ya kuupanda, wakati wafanyakazi wa kampuni hiyo, waliposhiriki kupanda majani, miti na kuweka mbolea katika bustani iliyopo katika Barabara ya Ali Hassan Mwinyi kuanzia Moroco hadi Namanga jijini Dar es Salaam jana, kuunga mkono kampeni ya utunzaji mazingira maarufu kama “mti wangu”, iliyozinduliwa hivi karibuni na Mkuu wa Mkoa huo, Paul Makonda. Kushoto ni Afisa Mazingira wa Manispaa ya Kinondoni, Awadh Jambo. 
 Wafanyakazi wa Airtel wakishiriki kupanda miti katika bustani iliyopo katika Barabara ya Ali Hassan Mwinyi kuanzia Moroco hadi Namanga jijini Dar es Salaam jana, kuunga mkono kampeni ya utunzaji mazingira maarufu kama “mti wangu”, iliyozinduliwa hivi karibuni na Mkuu wa Mkoa huo, Paul Makonda.

 Wafanyakazi wa Airtel wakishiriki kupanda majani katika bustani iliyopo katika Barabara ya Ali Hassan Mwinyi kuanzia Moroco hadi Namanga jijini Dar es Salaam jana, kuunga mkono kampeni ya utunzaji mazingira maarufu kama “mti wangu”, iliyozinduliwa hivi karibuni na Mkuu wa Mkoa huo, Paul Makonda.

Wafanyakazi wa Airtel wakishiriki kupanda majani katika bustani iliyopo katika Barabara ya Ali Hassan Mwinyi kuanzia Moroco hadi Namanga jijini Dar es Salaam jana, kuunga mkono kampeni ya utunzaji mazingira maarufu kama “mti wangu”, iliyozinduliwa hivi karibuni na Mkuu wa Mkoa huo, Paul Makonda.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...