Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla akiwa ameongozana na baadhi ya waendesha Bajaj wa eneo la Kabwe Jijini Mbeya, wakati alipofika kukutana nao ili kuwasikiliza, ambapo amesitisha kwa muda kuhamishwa kwa Waendesha Bajaj hao kituoni hapo mpaka hapo kituo kilichopendekezwa wao kwenda kifanyiwe marekebisho, pia ameagiza kuendelea kwa operesheni kwa Bajaji kufuata ruti na vituo walivyopangiwa ili kuepusha misongamano isiyo na lazima na kuhakikisha usafi unaendelea ili jiji la Mbeya liwe mfano wa kuigwa.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla akizungumza na vijana hao wanaojishughulisha na Uendeshaji wa Bajaj za abiria, eneo la Kabwe, Jijini Mbeya.
Baadhi ya madereva wa bajaji watumiao eneo la kabwe kuegesha bajaji zao wakizungumza na mkuu wa mkoa wa mbeya Amos Makalla (hayupo pichani). Na Mr.Pengo MMG-Mbeya.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...