Na Christina Mwagala, Dar es Salaam

MASHINDANO ya pili ya tuzo ya Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita la uandishi wa ushairi linatarajiwa kuanza Desemba 10 hadi 13 mwaka huu katika viwanja vya Karimjee.

Mratibu wa mashindani hayo Chatta Michael amesema lengo la mashindano hayo ni kutoa fursa kwa washiriki wa Kiswahili kushiriki katika kutafakari hali na maendeleo ya jiji kwa kutumia sanaa yao.

Amesema kwamba mbali na hilo, pia ni kuienzi historia ya jiji sambamba na kutambua mchango wa meya wa kwanza Mwafrika hayati Sheikh Kaluta Amri Abeid ambaye enzi zauhai wake alikuwa mshairi.

“ Mashindano haya tunawapa fursa pia ,kuijadili Dar es Salaam hali na mstakabali wa jiji lao na hivyo kuchangia katika kuhamasisha maendeleo ya jiji hili,na lugha ya kiswahili.

“ Kufufua sanaa ndani ya jiji, ili litumike kwa burudani ,elimu na maendeleo ya wakazi wote wa hapa, kuendeleza vipaji vya washairi wakongwe sambamba na kuibua vipaji vya washairi vijana ambao watakuwa ni wapya” amesema Chatta.

Aidha amefafanua kuwa mashindano hayo yataanza Desemba 19 hadi 20 mwaka huu, ambapo washindi wata tangazwa na hivyo mshindi wa kwanza atapatiwa shilingi 500,000, wapili shilingi 300,000, huku washindi nane wakipatiwa zawadi ya shilingi 100,000 kila mmoja.

Alisema mada kuu katika ushairi huo ni “Jiji la Dar es Salaam” ambapo mshairi atatakiwa kujadili mada ndogo inayohusiana na mada kuu, ikiwemo historia ya jiji, jiografia, utamaduni ,uchumi, mazingira ,sanaa na lugha .

Mbali na hivyo alieleza changamoto zilizopo katika jiji ,raha na karaha ,maendeleo wananchi wanaoishi katika jiji hili ambapo kila shairi litatakiwa kuzungumzia mada ndogo tofauti.

Hata hivyo mashindano hayo hufanyika kila mwaka ambapo mwaka huu yalifanyika Julai na kushirikisha washiriki 20 ambao washindi wa kwanza walipatiwa zawadi ya shilingi 500,000.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...