KAMPUNI ya Simu Tanzania (TTCL) imetoa laini maalumu za simu za mkononi kwa ajili ya wanafunzi wa vyuo zitakazokuwa na gharama nafuu za matumizi ya mtandao wa intaneti na ofa mbalimali za matumizi ya simu kuwawezesha wanafunzi kutumia mtandao kwa masomo yao. 

Akizungumzia ofa hiyo maalum iliyotangazwa kwenye semina kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Biashara Mlimani wa mwaka wa kwanza, Kaimu Mkurugenzi wa Biashara Kanda ya Dar es Salaam, Jane Mwajalebela alisema ofa hiyo kwa wanafunzi wa chuo imetolewa baada ya TTCL kusikiliza ombi la wanafunzi juu ya kupunguziwa gharama hasa kwenye intaneti kwa kuwa hutumia mtandao huo kujipatia masomo.

 Bi. Mwajalebela alisema laini hizo kwa wanafunzi ambazo zinajulikana kwa jina la 'Boompack', ambapo wanafunzi wa chuo watakuwa na fursa ya kupata huduma za vifurushi vya bei nafuu, ujumbe mfupi wa simu 'SMS' za kutosha na muda wa maongezi ambao kiujumla utarahisisha huduma kwa matumizi yao.

 "leo na Hivyo basi, tunapenda kuwatangazia kuwa TTCL inatoa laini za wanafunzi ambazo zinajulikana kwa jina la Boompack, wanafunzi wanafursa ya kupata huduma za vifurushi vya bei nafuu, SMS za kutosha na muda wa maongezi. Laini hii ni maalumu kwa wanafunzi na tumeanzisha ili kutoa fursa kwa wanafunzi kutumia intaneti kwa ajili ya kushughuli za kimasomo na kuimarisha mawasiliano miongoni mwa wanafunzi. 
Kaimu Mkurugenzi wa Biashara Kanda ya Dar es Salaam, Jane Mwajalebela akizungumza na baadhi ya wanafunzi wa Mwaka wa Kwanza wa Shule Kuu ya Biashara ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam 'Business School' (UDBS) (hawapo pichani). 
Baadhi ya wanafunzi wa Mwaka wa Kwanza wa Shule Kuu ya Biashara ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam 'Business School' (UDBS) (hawapo pichani). 
Semina ikiendelea kwa wanafunzi wa Mwaka wa Kwanza wa Shule Kuu ya Biashara ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam 'Business School' (UDBS) (hawapo pichani). Wa kwanza kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Biashara Kanda ya Dar es Salaam, Jane Mwajalebela. 
Baadhi ya wanafunzi wa Mwaka wa Kwanza wa Shule Kuu ya Biashara ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam 'Business School' (UDBS) wakisajili laini za wanafunzi ambazo zinajulikana kwa jina la Boompack. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Kila mtu anatext tu hapo. wakifeli watamlaumu muhadhiri hakufundisha vizuri. akiwaambie wazime simu watasema mnoko.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...