THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

WATUMISHI WAWILI WASIMAMISHWA KAZI KWA TUHUMA ZA UBADHIRIFU WA FEDHA MILIONI 42 MKOANI KIGOMA

Na Rhoda Ezekiel -Globu ya Jamii Kigoma,

MADIWANI wa Manispaa ya Kigoma Ujiji kupitia vikao vya kamati wamewasimamisha kazi watumishi wawili,ili kupisha uchunguzi wa upotevu wa takribani milioni 42 pamoja na matumizi mabaya ya fedha za miradi ya maendeleo kiasi cha shilingi milioni 250.

Maamuzi hayo yalichukuliwa mara baada ya kamati mbalimbali kujiridhisha na upotevu wa fedha kiasi cha milioni 42 ambazo zilihamishwa kutoka akaunti ya Amana na kupelekwa kwenye akaunti ya maendeleo na kutumiwa kulipa miradi mingine ya maendeleo iliyokuwa ikisimamiwa na Manispaa hiyo lakini pia matumizi mabaya ya fedha kiasi cha shilingi milioni 250 ambapo tume imeundwa ili kuchunguza zaidi tuhuma hizo.

Akitoa ufafanuzi Meya wa Manispaa hiyo Hussen Ruhava,mara baada ya maamuzi hayo alisema tume imeundwa kuchunguza watumishi wanne kati ya sita wamechukuliwa hatua za kinidhamu na kuwajibika kulipa fedha hizo huku kati ya hao wawili wamesimamishwa kazi kupisha uchunguzi na hatua za kisheria zitachukuliwa.

Ruhava aliiwataja walio simamishwa  kuwa ni Christina Nayingu ambae ni Mhasibu wa Manispaa na Michael  muhadhini wa Ndoliwa Muhadhina wasultani Ndoliwa na Dr Johni Tratra  kuwa watasimamishwa ili kupisha uchunguzi pindi utakapo kamilika,na  watatakiwa kulipa kiasi chote cha fedha kilicho tolewa.

Aidha Ruhava alisema licha ya maamuzi hayo lakini pia wameeleza kutokuwa na imani na Mkurugenzi wa Manispaa Judethadeus Mboya kutokana na kushindwa kukusanya mapato ipasavyo, asilimia kumi kutotolewa kwa vijana na wanawake, sanjari na asilimia 20 ya maendeleo kutokufika katika maeneo husika lakini pia sakata hilo lilimkumba na afisa mipango miji kushindwa kutekeleza maamuzi ya vikao vya madiwani na hivyo kuchukuliwa hatua za kinidhamu.

" hatutaki kufanya maamuzi ya kumuonea mtu, hatutaki kuchukua maamuzi ya kuwa karibisha watu, tunacho hitaji watumishi wafanye kazi ya kuwatumikia wananchi bila ubadhilifu wowote na kutenda haki ",alisema Ruhava
 
MADIWANI wa Manispaa ya Kigoma Ujiji wakiendelea na vikao vya kamati ,ambapo wamewasimamisha kazi watumishi wawili,ili kupisha uchunguzi wa upotevu wa takribani milioni 42 pamoja na matumizi mabaya ya fedha za miradi ya maendeleo kiasi cha shilingi milioni 250.