THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

WILAYA YA KAKONKO MKOANI KIGOMA HATARINI KUPOROMOKA KIUCHUMI

Na Rhoda Ezekiel Globu ya Jamii-Kigoma.

WILAYA ya Kakonko Mkoa wa Kigoma imeelezwa kuendelea kuporomoka kiuchumi kutokana na mzunguko mdogo wa fursa za kibiashara kupelekwa wilaya ya jiran na watumishi wa idara  inayohudumia  wakimbizi katika kambi ya mtendeli kuishi Wilayani Kibondo, hali inayo pelekea shughuli zao zote kufanyika Wilayani humo.

Kufuatia hali hiyo mkuu wa Wilaya Kanali Hosea Ndagala  alitoa  wito kwa watumishi  hao kutoa fursa za kiuchumi kwa wafanya biashara wa Wilaya ya Kakonko wakati wa ujenzi wa nyumba za kudumu za wakimbizi, lengo likiwa ni kuongeza mzunguko  wa kibiashara kwa Wananchi wanao izunguka kambi hiyo na kuacha tabia ya kutoa tenda zote za ujenzi kwa wafanya biashara wa Wilaya ya Kibondo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Wilayani humo, Ndagala alisema watumishi wengi wa Kambi ya mtendeli wamekuwa wakifanya biashara na wafanya biashara wa Kibondo,wakati kambi hiyo inahudumia wakimbizi katika Wilaya ya Kakonko hali inayo pelekea uchumi wa wananchi wa Kakonko waliotegemea kuupata kupitia kambi hiyo kuanzishwa kukosekana na kuhamia wilya nyingine ya Kibondo.

Ndagala alisema halmashauri ya Wilaya ya Kakonko ni halmashauri ambayo uchumi wake bado upo chini,unahitaji kuinuliwa hivyo akawaomba wafanyakazi wa kambi ya Mtendeli pamoja na shirika la kuhudumia wakimbizi UNHCR kutoa vipaumbele kwa  Wananchi wa Wilaya ya Kakonko ili kuinua uchumi wa Wilaya hiyo kwa kuwapatia ajira za ujenzi na ununuzi wa vifaa vya ujenzi kwa wafanya biashara wa Kakonko.

Hata hivyo Mkuu huyo aliwaomba watumishi wote  wa Kambi hiyo na mashirika yanayo hudumka wakimbizi kurudi kuishi Kakonko kwakuwa sababu iliyo kuwa ikiwapelekea waishi Kibondo ya kukosekana kwa Nyumba za kupanga Wilayani humo limekwisha Wananchi wamejitahidi kujenga nyumba zenue ubora ambazo wanaweza kupanga na kufanya kazi zao za kuhudumia wakimbizi wakiwa wilayani humo.