Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
Ligi
kuu ya Vodacom imeendelea leo katika viwanja mbali mbali huku katika
mchezo wa uliozikutanisha timu ya Azam Fc na Mbeya City ukimalizika kwa
suluhu ya timu hizo kushindwa kufungana.
Katika mchezo huo ambao ulianza saa moja usiku katika uwanja wa Chamazi Complex uliopo nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
Mchezo
huo ambao ulikuwa na ushindani wa aina yake kwa timu zote
zikishambuliana kwa vipindi na kucheza kwa kujiamini na kujituma
kuhakikisha wanajaribu kupata ushindi lakini bahati aikuwa upande
wowote.
Katika mchezo huo ambao mbeya City imeweza kucheza na
wachezaji wawili ambao washawahi kuchezea timu ya Azam ambao ni Mrisho
Ngassa na Zahoro Pazi na kuonyesha kuwa mwiba kwa timu hiyo kwa
kujaribu kulishambulia lango la timu yao ya zamani mara kadhaa.
Mrisho
Ngassa ambaye ameingia katika kipindi cha pili mara baada ya kutoka kwa
Tito Okelo ameweza kufanya mabadiliko makubwa katika safu ya
ushambuliaji kwa kuwa tishio katika lango la Azam Fc.
Ngasa
ambaye ameweza kucheza kwa kuonyesha uzoefu wa hali ya juu kwa kuweza
kusaidia upande wa kati na kuwa kivutio kikubwa kwa mashabiki kutokana
na staili yake ya mchezo .
Kikosi cha Mbeya City kilichoanza leo
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...