Na Mwamvua Mwinyi,Bagamoyo
MBUNGE wa jimbo la Bagamoyo,dk.Shukuru Kawambwa ameelekeza nguvu zake katika ujenzi wa madarasa katika shule mbalimbali jimboni humo ambapo amechangia zaidi ya mifuko 1,000 ya saruji.
Aidha ametoa zaidi ya sh.mil.10 kuchangia vikundi viwili vya ujasiriamali kwenye kila kata kwa ajili ya kukopeshana ambapo kati ya vikundi hivyo vimewezeshwa sh.mil.1 hadi mil.1.5.
Hayo aliyasema ,kijiji cha Mwavi,Mkenge na Fukayose wakati wa ziara yake inayolenga kupeleka mrejesho kwa wananchi kuhusiana na hatua anazozichukua kufuatilia kero zao zinazowakabili.
Dk.Kawambwa alisema jimbo hilo lina jumla ya kata 11 na kila kata ameichangia kati ya mifuko 100-150 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa .
Alieleza kuwa amehakikisha mfuko wake wa jimbo unaunga mkono juhudi za wananchi kwenye ujenzi huo na kuwezesha wajasiriamali.
Mbunge huyo alisema,ameamua kuchukua hatua hiyo baada ya kuona bado shule nyingi zinapambana na changamoto ya uhaba wa madarasa na vikundi kukosa mitaji.
Hata hivyo,dk.Kawambwa aliahidi kutoa matofali 1,000 katika kitongoji cha Kalimeni na kwa kijiji cha Kitopeni ameshawapa ardhi yenye heka 6 na fedha kwa ajili ya kujenga shule na tayari wameanza .
“Nimeona suala la madawati limemalizika vizuri kwa ushirikiano wa wadau,halmashauri na ofisi ya wilaya ya Bagamoyo,tumevuka kwa hili lakini tatizo ni majengo “
“Nitaelekeza nguvu zangu katika ujenzi huu kulingana na uwezo uliopo pamoja na kusupport akina mama na vijana kwenye vikundi vyao”alisema dk.Kawambwa.
Aliiomba jamii washirikiane kwa pamoja kwenye ujenzi wa madarasa ili kufanikisha lengo lao la kuondokana na upungufu wa madarasa.
MBUNGE wa jimbo la Bagamoyo Dkt. Shukuru Kawambwa akizungumza na wanachama wa vikundi vya ujasiriamali vya jipe moyo na kiroho safi,vilivyopo Mwavi kata ya Fukayose,wakati wa ziara yake aliyoianza jimboni hapo.
 
 MBUNGE wa jimbo la Bagamoyo Dkt. Shukuru Kawambwa akizungumza na baadhi ya wananchi wa kijiji cha Mkenge kata ya Fukayose,wakati wa ziara yake aliyoianza jimboni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...