WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka watendaji wa Serikali wahakikishe wanawasimamia vizuri wakandarasi wanaojenga miradi mbalimbali nchini ikiwemo ya barabara ili viwango vyake vifalingane na thamani halisi ya fedha zinazotolewa.

Ametoa kauli hiyo leo (Jumatano, Januari 11, 2017) wakati akizundua mradi wa ujenzi wa barabara ya Kwerekwe/Fuoni yenye urefu wa kilomita 4.01 iliyogharimu sh. bilioni 10.07 zilizotolewa na Mfuko wa Barabara. Ujenzi huo ni utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2015.

Waziri Mkuu amezindua barabara hiyo kwa niaba ya Mheshimiwa Rais Dk. John Magufuli ikiwa ni sehemu ya sherehe za maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

Amesema Serikali inatumia fedha nyingi katika miradi ya ujenzi wa barabara hivyo watendaji wake hawana budi kuhakikisha miradi hiyo inalingana na thamani halisi ya kiwango cha fedha kinachotolewa.

Aidha, Waziri Mkuu amewataka watendaji hao kuwaelimisha wananchi umuhimu wa kulinda na kuhifadhi miundombinu hiyo na kuwachukulia hatua wote watakaobainika kufanya uharibifu ikiwemo uchomaji wa matairi katikati ya barabara.

Pia amewataka wananchi kutojenga majengo ya kudumu katika hifadhi ya barabara ili kuepusha usumbufu pale Serikali inapotaka kuyatumia maeneo hayo. “Lazima wananchi wazingatie sheria ya hifadhi ya barabara,”

“Serikali imedhamiria kuboresha mawasiliano kwa kujenga barabara zetu kwa kiwango cha lami. Hatatutakubali kuona mtu anaharibu miundombinu hii tunayoijenga kwa gharama kubwa ikiharibiwa. Lazima tuilinde ili iweze kutunufaisha wote,” amesema.

   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizindua barabara ya Mwanakwerekwe hadi Fuoni yenye urefu wa kilomita 4.1 iliyopo Zanzibar Januari 11, 2017.  Kushoto ni  Waziri wa  Ujenzi,  Mawasiliano na  Usafirishaji, Ali Karume . (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifurahia baada ya kuzindua barabara yenye urefu wa kilomita 4.1  ya kutoka Mwanakwerekwe hadi Fuoni Zanzibar ikiwa ni moja ya shughuli za sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar, Januari 11, 2017.  Katikati ni Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Pili wa rais wa Zanzibar, Mohammed Abood na Kulia ni  Mkuu wa mkoa waMjini Magharibi, Mohammed Mahmoud. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim  Majaliwa akiwapungia wananchi wa Zanzibar wakati  alipowasili kwenye eneo la  Barabara ya Mwanankwerekwe  hadi Fuoni kufungua barabara hiyo yenye urefu wa Kilomita 4.1 Januari 11, 2017. Kushoto ni Waziri wa Ujenzi, , Mawasiliano na Usafirishaji, Ali Karume. (Picha na  Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Baadhi ya wananchi wa Zanzibar wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza baada ya kuzindua barabara ya Mwanakwerekwe hadi Fuoni yenye urefu wa Kilomita 4.1 ilyopo Zanzibar Januari 11, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akishiriki katika dua iliyosomwa baada ya kuzindua barabara ya Mwanakwerekwe hadi Fuoni yenye urefu wa Kilomita 4.1 iliyopo Zanzibar Januari 17, 2017.Wengine pichani kutoka kushoto ni Spika wa Baraza la Wawakilishi,   Zubri Ali Maulid, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Mohammed Mahmoud na kulia ni Waziri wa Ujenzi, Mawsiliano na  Usafirishaji, Ali Karume. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

SOMA ZAIDI HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...