Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ametahadharisha kwamba uzembe wa aina yoyote  unaoweza kufanywa  na Kikosi cha Zimamoto na Uokozi wakati inapotokea dharura kwa bahati mbaya unaweza kukimbiza huduma za ndege za Kimataifa zinazotumia uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Zanzibar.
Alisema  umuhimu wa Kikosi hicho kuwepo katika maeneo ya Viwanja vya ndege hata Bandarini kwa ajili ya kutoa huduma za uokozi wa masuala ya dharura ni muhimi na mkubwa kwa Uchumi wa Taifa hili.

Balozi Seif Ali Iddi alitoa kauli hiyo wakati wa ufunguzi wa Kituo cha Zimamoto na Uokozi cha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume ikiwa ni miongoni mwa shamra shamra za maadhimisho ya sherehe za kutimia miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Mwaka 1964.

Balozi Seif alisema  Serikali imekuwa ikichukuwa jitihada mbali mbali za kukiimarisha Kikosi hicho cha Zimamoto ili kiende sambamba  na Teknalojia  ya kisasa pamoja na kufikia  kutoa huduma zenye viwango vya  Kimataifa.
Alisema Idara ya  Zimamoto na uokozi  ni nyenzo muhimu katika Taifa lolote Duniani, hivyo ni vyema kwa watendaji wa Taasisi hiyo   wakaandaliwa utaratibu muwafaka wa kupatiwa mafunzo ya mara kwa mara  ndani na nje ya nchi.

  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akikagua gari jipya la zimamoto baada ya  kuzindua rasmi Jengo la Kituo cha kikosi cha zimamoto na uokozi cha uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abeid Aman Karume Zanzibar ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya sherehe za miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 Gari jipya la Kikosi cha zimamoto na Uokozi likiwa ni moja  miongoni mwa magari Manne yaliyonunuliwa na Serikali Kuu kwa ajili ya Kikosi cha zimamoto na Uokozi Zanzibar.
 Kamishna wa Kikosi cha Zimamoto na Uokozi Zanzibar Kamishna Ali Abdulla Malimus akitoa Taarifa ya ujenzi wa Kituo cha Zimamoto cha Uwanja wa Ndege wa Zanzibar.
 Katibu Mkuu Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ  Bibi Radhia Rashid Haroub akizungumza kwenye uzinduzi wa Jengo la Kituo cha Zimamoto na Uokozi cha Uwanja wa Ndege wa Zanzibar.
Balozi Seif Ali Iddi  kati kati waliokaa akiwa katika picha ya pamoja na Baadhi ya Mawaziri wa SMZ, Viongozi wa  Taasisi zinazosimamiz sekta ya mawasiliano pamoja  na Maafisa wa Kikosi cha Zimamoto na Uokozi mara baada ya uzinduzi wa jengo la Kikosi cha Zimamoto Uwanja wa Ndege wa Zanzibar. Picha na – OMPR – ZNZ.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...