Wizara ya Nishati na Madini kupitia Mradi wa Kuwajengea Uwezo Wataalam wa Nishati na Tasnia ya Uziduaji (CADESE: Capacity Development in the Energy Sector and Extractive Industries), inatarajia kuanzisha mfumo wa uhifadhi data kwa ajili ya nishati jadidifu ujulikanao kama Tanzania Renewable Energy Management Information System (TREMIS) utakaowezesha wawekezaji ndani na nje ya nchi kubaini fursa za uwekezaji zilizopo katika sekta ya nishati jadidifu.
Hayo yameelezwa na Msimamizi wa Mradi wa Kuwajengea Uwezo Wataalam wa Nishati na Tasnia ya Uziduaji (CADESE), Paul Kiwele katika ziara ya maandalizi ya mfumo huo jana, Kahama mkoani Shinyanga.
Mtaalam
kutoka Sehemu ya Nishati Jadidifu- Idara ya Nishati, Wizara ya Nishati na
Madini, Mhandisi Stephan Kashushura (kushoto) akizungumza na mtaalam kutoka kampuni ya vifaa vya umeme jua ya Mobisol,
Devis Mtete (kulia) mjini Kahama mkoani Shinyanga tarehe 11 Januari, 2017
Mtaalam
kutoka Sehemu ya Nishati Jadidifu- Idara ya Nishati, Wizara ya Nishati na
Madini, Mhandisi Stephan Kashushura (kushoto) akizungumza na mtaalam kutoka kampuni ya vifaa vya umeme jua ya Mobisol,
Devis Mtete (kulia) mjini Kahama mkoani Shinyanga tarehe 11 Januari, 2017
Mtaalam
kutoka kampuni ya vifaa vya umeme jua ya Zola, Omary Raymond (katikati)
akielezea shughuli za kampuni yake kwa Mtaalam kutoka Sehemu ya Nishati
Jadidifu- Idara ya Nishati, Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Stephan
Kashushura (kulia). Kushoto ni Msimamizi wa Mradi wa Kuwajengea Uwezo Wataalam wa Nishati na Tasnia ya
Uziduaji (CADESE) chini ya Wizara ya Nishati na Madini, Paul Kiwele.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...