Naibu waziri wa habari, utamaduni, sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura wikiendi hii  aliongoza wananchi wa mkoa wa Iringa katika mazoezi ya pamoja yaliyofanyika Uwanja wa michezo wa Samora Machel kupambana na magonjwa kama kisukari na shinikizo la damu. 
Mazoezi hayo ambayo yalianzia ofisi ya mkuu wa mkoa yalishirikisha viongozi, watumishi wa taasisi mbalimbali pamoja na wanachi. Mkuu wa mkoa wa Iringa Bi Amina Masenza alimshukuru Naibu Waziri kwa kutenga muda wake na kujumuika na wana Iringa. Akihitimisha mazoezi hayo Mhe wambura alisisitiza suala la lishe bora na kuwaasa watanzania kugeuza mazoezi kuwa utamaduni. “ Kila mtanzania popote alipo aanze sasa kuona mazoezi ni moja ya mila na desturi yake au utamaduni” 
Mkuu wa wilaya ya Iringa Mhe. Richard Kasesela alisisitiza kuwa mazoezi hayo yataendelea kila Jumamosi kasoro Jumamosi ya usafi, na kwamba arehe 4/2/2017 mazoezi haya yatafanyika tena ambapo anatarajiwa kualikwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Mhe Ummy Mwalimu kuja kushiriki mazoezi. 
Wananchi wa rika mbali mbali walitembea pamoja na viongozi wa mkoa na wilaya. Akihojiwa kamanda wa Polisi wa Mkoa Kamishna Msaidizi wa Polisi Mjengi alisema amaefarijika kuona mwamko wa mazoezi “ Sisi (polisi) tunafanya mazoezi karibu kila siku mwamko huu ukiendelea Iringa hakutakuwa na magonjwa kabisa pia itawajenga wananchi kujilinda na uhalifu.”
 Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akiongoza jinsi ya kufanya mazoezi ya viungo katika Uwanja wa Samora Machel
  Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akiongoza jinsi ya kufanya mazoezi ya viungo katika Uwanja wa Samora Machel
  Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akiongoza jinsi ya kufanya mazoezi ya viungo katika Uwanja wa Samora Machel
 Naibu waziri wa habari, utamaduni, sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akiongoza mazoezi
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akiwa na  kamanda wa Polisi wa Mkoa Kamishna Msaidizi wa Polisi Mjengi kwenye mazoezi hayo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...