Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 11 Januari, 2017 ameanza ziara ya siku mbili mkoani Simiyu kwa kuwataka wananchi wa mkoa huo na Tanzania kwa ujumla kuwapuuza  watu wanaoendesha siasa alizozitaja kupitwa na wakati kwa kutumia baadhi ya vyombo vya habari kutangaza kuwa Tanzania inakabiliwa na njaa badala ya kuwahamasisha wananchi kufanya kazi
Dakta Magufuli amesema hayo wakati akizungumza na wananchi katika uwanja wa Shule ya Msingi Somanda mara baada ya kuweka jiwe la Msingi katika  Hospitali ya Mkoa wa Simiyu na kufungua barabara ya Lamadi hadi Bariadi yenye urefu wa kilomita 71.8 iliyogharimu zaidi ya shilingi Bilioni 90.
Amesema kumekuwepo na baadhi ya wanasiasa na wafanyabiasha ambao wamekuwa wakiwahamisisha wananchi na kutumia baadhi ya vyombo vya habari kutangaza baa la njaa wakati wanasiasa hao hao ndio waliopitisha Bungeni kutaka nchi iuze chakula nje ya nchi na sasa hao hao wanatangaza baa la njaa.
'' Baadhi ya wanasisa walizungumza Bungeni kutaka wananchi waruhusiwe kuuza chakula nje ya nchikwa kuwa kuna chakula cha kutosha leo hii hao hao wanatumia baadhi ya vyombo vya habari kutanga baa la njaa''  . KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
 Rais Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe  na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Antony Mtaka pamoja na Waziri wa Ujenzi Profesa Makame Mbarawa kuashiria ufunguzi wa barabara ya Barabara ya Bariadi-Lamadi yenye kilometa 71.8.
 Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiweka jiwe la ufunguzi wa barabara ya Bariadi-Lamadi yenye kilometa 71.8 wengine katika picha ni  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Antony Mtaka, Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano Luhaga Mpina, Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, Mwenyekiti wa CCM Simiyu Titus Kamani na Mbunge wa Bariadi Andrew Chenge.
 Rais Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi wa Bariadi kabla ya kufungua rasmi barabara ya Bariadi-Lamadi, katika mkoa wa Simiyu.
 Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wakazi wa Bariadi mara baada ya kumaliza kufungua barabara ya Bariadi-Lamadi yenye urefu wa kilometa 71.8. Picha na IKULU

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...