Na. Aron Msigwa – NEC, Zanzibar.

Hatimaye wananchi wa Jimbo la Dimani visiwani Zanzibar waliojiandikisha katika Daftari la Kudumu la Mpiga leo wamejitokeza kwa wingi katika vituo mbalimbali kupiga kura kumchagua Mbunge atakayewawakilisha kwa kipindi cha miaka miaka 4.

Zoezi la upigaji wa Kura katika vituo mbalimbali lilianza majira ya saa 1 asubuhi  likifanyika kwa hali ya Amani na Utulivu huku baadhi ya wananchi waliojitokeza kupiga kura wakipongeza maandalizi mazuri yaliyofanywa na Tume ya Taifa ya Uchaguzine (NEC)  kufanikisha Uchaguzi huo.

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji wa Rufaa, Mhe. Semistocles Kaijage akizungumza kuhusu mwenendo wa Uchaguzi huo mara baada ya kutembelea vituo  vya kupigia kura katika jimbo hilo na  kuzungumza  na Mawakala wa Vyama vya Siasa waliokuwepo vituoni, Waangalizi wa Uchaguzi na Wasimamizi wa Uchaguzi  huo amesema Tume imeridhishwa na kazi nzuri  iliyokuwa ikiendelea katika vituo mbalimbali vya kupigia Kura.

Viongozi wa Tume tumetembelea vituo mbalimbali vya kupigia Kura katika jimbo la Dimani; tumeona wenyewe upigaji wa Kura unaendelea vizuri, tumewauliza Mawakala, Watazamaji na Wasimamizi wa Vituo vya Uchaguzi  kila mmoja amesema Uchaguzi unakwenda vizuri, nachoweza kuwaambia watanzania Uchaguzi Dimani unakwenda Vizuri” Amesema Jaji Kaijage.

Amesema Wasimamizi wa Uchaguzi katika Jimbo hilo wanaendelea kufanya kazi zao kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Maadili pia kushughulikia kwa haraka changamoto zilizokuwa zikijitokeza katika  baadhi ya vituo vya kupigia Kura.

 Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji wa Rufaa Mhe. Semistocles Kaijage (Katikati) akizungumza na Msimamizi kituo cha Dimani Bi. Abdu Simai Haji leo wakati zoezi la upigaji kura likiendelea katika jimbo la Dimani.
 Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji wa Rufaa Mhe. Semistocles Kaijage (Katikati) akizungumza na waandishi wa Habari wa Zanzibar kutoa tathmini ya hali ya Uchaguzi mara baada ya kuetembelea vituo mbalimbali vya kupigia kura katika jimbo la Dimani leo. 
 Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji wa Rufaa Mhe. Semistocles Kaijage (wa pili ) akiwa ameambatana na Baadhi ya Watendaji wa NEC na  Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi Bi. Idaya Selemani Hamza (wa Kwanza) akiwasili katika kituo cha Kupigia Kura cha Kombeni katika jimbo la Dimani kuangalia maendeleo ya  Upigaji wa Kura leo.
 Mmoja wa Wananchi katika jimbo la Dimani akipiga Kura yake kumchagua Mbunge katika jimbo la Dimani leo.
 Baadhi ya Wangalizi wa Uchaguzi katika jimbo la Dimani wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa Uchaguzi mdogo wa Ubunge katika jimbo la Dimani leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...