AWAPA SIKU 14, WAFANYA BIASHARA NJE YA SOKO KUHAMIA NDANI YA SOKO

Na Anthony John Glob Jamii. 
MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi ameendelea na ziara ya kutembelea Kata za wilaya ya kinondoni, ikiwa siku ya pili ya ziara yake mkuu wa wilaya ametembelea kata Mzimuni, akiwa katika soko la Magomeni, ametoa siku 14 kwa uongozi wa soko hilo kuhakikisha wanaondoa baa na ghala vilivyopo katikati ya soko hilo.

Akiwa ndani ya soko hilo, Hapi alisema inasikitisha kuona hata wamiliki wa ghala hizo hawafahamiki.Alisema uwepo wa ghala na baa katikati ya soko hilo inasababisha kuwanyima fursa wafanyabiashara walio wengi hasa wale wadogo.

"Ninatoa siku 14 kwa viongozi wa soko na manispaa kuhakikisha wanaaondoa maghala haya kwani inaonyesha ni ya wafanyabiashara wakubwa hivyo waende kwa wenzao hapa hapawafai,"alisema Hapi.

Sambamba na hilo mkuu huyo ametoa siku 14 nyingine kwa wafanyabiashara wanaofanya biashara nje ya soko hilo kurejea ndani ya.soko.Alisema sheria zipo wazi na hakuna aliyejuu ya sheria zaidi ya kuzingatia sheria hizo.

"Hakuna aliyeruhusu wafanyabiashara wengine kufanya biashara nje ya soko,  hivyo naagiza ndani ya siku 14 wote mhamie ndani kwa sababu mnaleta usumbufu kwa wengine na kuleta malalamiko,"alisema Hapi.

Baadae mkuu wa wilaya alifanya mkutano wa adhara katika shule msingi Mikumi, katika mkutano huo wananchi waliuliz maswali mbali mbali lakini kero kubwa imeonekana kuwa viongozi wao sio waaminifu hukusanya pesa kwa wananchi lakini hafanyi yaliyokusudiwa, mkuu wa wilaya akijibu hoja hiyo ameagiza viongozi wote kutoa risit za EFD kwa kila malipo yanapofanyika

 MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi akizungumza na Wananchi mapema leo kwenye muendelezo wa ziara yake jijini Dar
  MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi akisikiliza kero mbalimbali za Wananchi na kuzitafutia ufumbuzi
Wanachi wa Mzimu wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...