Benny Mwaipaja, WFM, Tunduma

KITUO cha Pamoja cha Forodha cha mpaka kati ya Tanzania na Zambia (Tunduma/Nakonde) kimeanza rasmi kutumika licha ya kukabiliwa na msongamano mkubwa wa magari unaotakiwa kupatiwa ufumbuzi wa haraka.

Kituo hicho kimeanza kufanyakazi tangu Februari mosi mwaka huu, ambapo watumiaji wa mpaka huo watakuwa wakihudumiwa upande mmoja wa mpaka badala ya utaratibu uliokuwa ukitumika awali ambapo watumiaji walilazimika kukaguliwa mizigo yao kila upande hatua iliyokuwa ikichelewesha biashara katika mpaka huo

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Khamis Shaaban, Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof. Adolf Mkenda na Naibu Waziri wa mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Hassan Simba Yahya, wameeleza kuridhishwa na kazi inayofanyika mpakani hapo kupitia mfumo huo mpya.

Hata hivyo baadhi ya madereva wanaosafirisha bidhaa kupitia mpaka huo wa Tunduma na Nakonde, pamoja na kupongeza utaratibu huo mpya, wameiomba Serikali iwasiliane na upande wa Zambia, ili waongeze kasi ya kuruhusu malori kuendelea na safari yanapofika mpakani hapo bila kucheleweshwa ili kwenda sambamba na kasi ya upande wa Tanzania, ambao umeboresha kwa kiwango kikubwa utoaji wa huduma.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof. Adolf Mkenda, amesema kuwa makubaliano yaliyofikiwa kati ya Serikali na watoa huduma katika mpaka huo yalikuwa ni kuwahudumia wadau wanaotumia mpaka huo kwa muda usiozidi siku moja na kuwataka madereva wa malori wanaokwazwa kuwasiliana na mamlaka zinazohusika.
Kaimu Afisa Uhamiaji Mfawidhi wa Kituo cha mpakani Tunduma/Nakonde, Bw. Tabaran Mzee, (aliyevaa sare za uhamiaji), akieleza namna idara hiyo ilivyoanza utekelezaji wa uanzishwaji wa Kituo cha Pamoja cha Forodha kati ya Tanzania na Zambia, ambapo wafanyakazi wa idara hizo kutoka nchi hizo mbili wanafanyakazi katika jengo moja kila upande wa nchi ili kuboresha ufanyaji biashara mpakani.
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji (anayeshughulikia biashara na uwekezaji), Prof. Adolf Mkenda, akionesha kibao chenye namba za simu kilichowekwa Idara ya Forodha katika mpaka wa Tunduma/Nakonde zitakazotumiwa na wadau endapo watakuwa na malalamiko yoyote, lengo likiwa ni kuboresha huduma katika mpaka huo ambapo huduma ya pamoja ya forodha kati ya Tanzania na Zambia imeanza kutolewa rasmi tangu Februari mosi mwaka huu.
Makatibu Wakuu wa Wizara ya Fedha, Viwanda, na Mambo ya Ndani, wakizungumza na Afisa Forodha wa Zambia aliyeko katika Kituo cha Forodha cha Tunduma upande wa Tanzania, baada ya Ujumbe huo wa Serikali kutembelea mpaka huo kukagua shughuli za biashara ikiwa ni siku kadhaa baada ya kuanza rasmi kwa huduma ya Kituo cha Pamoja cha Forodha katika mpaka huo wa Tunduma/Nakonde (Tanzania na Zambia).
Mkuu wa Wilaya ya Momba mkoani Mbeya Bw. Juma Irando (aliyenyoosha kidole) akieleza jambo baada ya ujumbe wa Serikali ukiongozwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Khamis Shaaban, ulipotembelea mpaka huo kukagua shughuli za biashara baada ya kuanza rasmi kwa huduma za Kituo cha Pamoja cha Forodha mpakani Tunduma/Nakonde.
Kituo cha Uhamiaji na Forodha cha Tanzania kilichoko kwenye jengo la Zambia upande wa Nakonde, baada ya kuanzishwa kwa Kituo cha pamoja cha Forodha cha Mpakani mwa Tanzania na Zambia (Tunduma/Nakonde).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...