Na Rhoda Ezekiel-Globu ya Jamii, Kigoma.
JESHI
la Polisi Mkoani Kigoma limekamata Wahamiaji haramu 226, Kete za bangi
191, Heroin kete tano , pombe ya moshi lita 300 na silaha aina ya gobore
moja, katika msako wa kupambana na dawa za kulevya, wahamiaji haramu
pamoja na uhalifu uliofanyika kwa kipindi cha Wiki moja ili kuhakikisha
Mkoa upo salama.
Akitoa
taarifa ya Msako huo leo mbele ya Waandishi wa habari Mkoani humo ,
Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoani Kigoma, DCP Fredinand Mtui alisema
kuanzia Februal 2 mwaka huu jeshi la polisi Mkoani humo lilianza Msako
wa kuhakikisha wanakomesha vitendo vya uhalifu, matumizi ya Dawa za
kulevya na uuzaji pamoja na wahamiaji haramu wanaoingia Nchini bila
vibali, hali inayo sababisha uhalifu kuongezeka kutokana na vitendo
hivyo.
Mtui
alisema kuwa mnamo februali 16 ulifanyika msako na kufanikiwa
kuwakamata wahamiaji haramu 203 katika kijiji cha Mganza Wilayani Kasulu
wakitokea nchini Burundi wakiwa katika mashamba ya Wakulima,alisema na
kuongeza kuwa Kigoma mjini walikamatwa wahamiaji 7 , kibondo 9 na
Buhigwe 7a na jumla yao ni wahamiaji 226 ambao waliingia nchini Kinyume
na utaratibu huku wakipokelewa na Wenyeji na wanawahifadhi.
Alisema
Wengi wa wahamiaji hao wanatoroka Nchini mwao wakiwa wamefanya uhalifu
na wanakuja Nchini na wanapokelewa na wenyeji na wanawatumia katika
kilimo pia wengi wao ndio wanaotumika kifanya uhalifu mkoani humo ambapo
Kamanda Mtui aliwaomba Wananchi kuacha kuwapokea Wahamiaji hao ambao
wengi wao husababisha madhala makubwa katika maeneo yao.
Aidha
Mtui alisema kwa upande wa madwa ya kulevya jeshi la polisi lilikamata
katika Wilaya ya Kigoma kete za bhangi 191 sawa na gram10 pamoja na
Heroin kete tano, Kasulu walikamata robo eka na gram 500 , kibondo miche
10 na Kakonko miche 60 ,kilo moja ya Bhangi madawa hayo yalikuwa
yakiuzwa kwa vijana ambao wengi wao hawafanyi kazi na wanaendelea
kufanya vitendo vya uhalifu.
"
tumeweza kutoa kipaumbele katika uhalifu unao tusumbua kwa kiasi
kikubwa Mkoani Kigoma ambao ni wahamiaji haramu , na matumizi ya Dawa za
kulevya, kwa mujibu wa upelelezi tulio ufanya wengi wanaoingia bila
vibali ni wale wahalifu wanao kimbia mikono ya sheria kutokana na
uhalifu kama tunavyo fahamu muahalifu hawezi kuacha uhalifu kiurahisi
ndio ambao wanakuja kiendelea kufanya uhalifu niwaombe Wananchi kuacha
kupokea Wahamiaji halamu kwasababu kwa sasa tutakae mkamata anawahifadhi
wahamiaji halamu watafikisha mahakamani", alisema Kamanda Mtui.
Alisema
katika msako huo zilipatikana idadi ya kesi katika msako huo ni kesi ya
uhamiaji haramu ni nane , kupatikana pombe ya moshi kesi 11, kupatikana
Bhangi kesi tisa , kupatikana na silaha kesi moja na kupatikana na
heroini kesi moja, watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani ilikuweza
kujibu tuhuma zinazo wakabili.
Kamanda
wa Jeshi la polisi Mkoani Kigoma, DCP Fredinand Mtui akizungumza na
baadhi ya wandishi wa habari mapema leo kuhusiana na operesheni
walioifanya ya kupambana na dawa za kulevya, wahamiaji halamu pamoja na
uhalifu iliofanyika kwa kipindi cha Wiki moja ili kuhakikisha Mkoa upo
salama.
Madumu ya pombe ya moshi (gongo),lita 300 zikiwa zimekamatwa
Kete za bangi 191 zikiwa zimekamatwa
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...