Jeshi la Polisi mkoa wa Mbeya limeendelea kufanya misako, operesheni na doria zenye tija katika maeneo mbalimbali ili kudhibiti uhalifu na wahalifu na limekuwa likishirikiana na wananchi na wadau wengine katika jitihada hizo za kukabiliana na uhalifu na wahalifu na kupata mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kupungua kwa matukio makubwa ya uhalifu. 

Kufuatia mapambano yanayoendelea nchi nzima dhidi ya watu wanaojihusisha na uuzaji na utumiaji wa dawa za kulevya, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limefanya misako na Mafanikio yaliyopatikana katika Misako ni kama ifuatavyo:-




KUKAMATA WATUHUMIWA WANAOJIHUSISHA NA BIASHARA YA UUZAJI/USAMBAZAJI WA DAWA ZA KULEVYA.



Mnamo tarehe 11.02.2017 majira ya saa 02:00 usiku, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya lilifanya misako katika maeneo ya Manga na Nsalaga – Uyole na kukamata watuhumiwa wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya ikiwa ni pamoja na wauzaji, wasambazaji na watumiaji [mateja]. Watuhumiwa waliokamatwa kutokana na kujihusisha ba usambazaji na uuzaji wa dawa za kulevya ambao ni 1. SHABAN RAMADHAN [40] Mkazi wa Uyole 2. RASHID YASIN [35] Mkazi wa Nonde 3. RODA MWAMBERA [60] Mkazi wa Mama John 4. MRISHO RAMADHAN [22] Mkazi wa Airport - Iyela na 5. MUSSA KIMBE [33] Mkazi wa Nonde.



Watuhumiwa wote wapo mahabusu na mahojiano zaidi yanaendelea ili kubaini mtandao mzima wa watu wanaojihusisha na dawa za kulevya.



KUKAMATA WAUZAJI/WASAMBAZAJI WA DAWA ZA KULEVYA.



Aidha kufuatia misako iliyofanyika kuanzia tarehe 19.01.2017 hadi tarehe 09.02.2017 katika maeneo mbalimbali Mkoani Mbeya, Watuhumiwa wawili walikamatwa katika matukio mawili tofauti wakiwa na dawa za kulevya.



Katika msako wa kwanza uliofanyika maeneo ya Ilemi Jijini Mbeya, HENRY MWAMFUPE [19] Mkodishaji Baiskeli na Mkazi wa Ilemi alikamatwa akiwa na kete 03 za dawa za kulevya aina ya Heroine.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...