Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limewatahadharisha wanachama na wapenzi wa klabu ya Yanga, kutobeba mabango ya kukashifu Serikali wala kiongozi yeyote wa nchi kesho wakati wa mchezo wa marudiano na Ngaya Club de Mde ya Comoro.

Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas alisema jana kwamba wanawaonya mashabiki wa soka nchini waliopanga kuleta vurugu na kuonyesha viashiria vya kukashifu viongozi wa soka na Serikali katika mchezo wa wa kesho na wa Februari 25 dhidi ya Simba, wasithubutu kabisa kwani vyombo vya dola vinawajibika katika kushughulika nao.

Lucas amesema hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa yeyote atakayethubutu kufanya kitu cha namna hiyo na kwamba kutakuwa na ulinzi mkali kesho Uwanja wa Taifa kwa ajili hiyo na kuwasihi mashabiki kuacha dhana hiyo kabisa na waje uwanjani kuja kushangilia mpira na kuipa sapoti timu yao

Yanga watakuwa wenyeji wa Ngaya katika mchezo wa marudiano Raundi ya Awali Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo mechi ya awali waliweza kutoka na ushindi wa goli 5-1 na hata hivyo tayari uongozi wa klabu ya Yanga ulishawasihi mashabiki wa timu hiyo kwenda kwa amani uwanjani na kutokufanya vurugu ya aina yoyote.

Kiingilio cha chini katika mchezo wa kesho kitakuwa Sh. 3,000 Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, VIP A Sh 20,000, VIP B Sh 10,000 na VIP C Sh 10,000.

Mechi hiyo itachezeshwa na marefa kutoka Uganda ambao ni Alex Muhabi Nsulumbi atayekapuliza filimbi uwanjani, akisaidiwa na washika vibendera Ronald Kakenya na Lee Okello.

Refa wa Akiba atakuwa Brian Nsubuga Miro huku Kamishna akitokea Afrika Kusini ambaye ni Monnyenyone Lucas Nhlapo.



Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...