Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamiii 

WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amefanya ziara katika maduka ya filamu za nje ambazo zinaingizwa nchini bila kuwa na utaratibu na kusaisababishia serikali kukosa filam na kushusha soko la filam zinazozalishwa nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari katika operesheni iliyoshirikisha vyombo vitano vinavyohusiana na kazi ya filam, Nape amesema filam zinaingizwa nchini zinafanya maadili kuharibika kuanzia mashuleni kwa kuwepo ushonga pamoja na ndoa za jinsia moja iliyotokana na watu kuangalia filam hizo.

Katika operesheni hiyo wameweza kukuta duka lenye Filamu za nje ni nyingi ambazo zinauzwa Dar es Salaam na kusambazwa mikoani pamoja na nje ya nchi huku maadili ya nchi yakiangamia kwa ajili ya watu wachache.

Amesema kuwa baada ya operesheni katika maduka wataingia mitaani na watu watakaokutwa wanauza hizo filamu za nje ambazo hazina stika za TRA watachukuliwa kama sehemu ya wanaohujum uchumi wa nchi.

''Hatuwezi kuwa tunawaachia watu wanafanya vitu ambavyo vinaharibu maadili na kuisababishia serikali kukosa mapato na watu wengine tukakaa kimya huku wengine wakilia hali mbaya ya soko kutokana na kuwepo kwa filamu hizi tutawabana mpaka mwisho ''amesema Nape.

Filamu hizo zimepatikana katika hoteli ya Buttefly inayomilikiwa na Fili Ulaya Mdoro ambaye ndio anafanyabiashara hiyo ya kuingiza filamuza nje bila kufuata utaratibu .

Nape amesenma kuwa watafutia leseni watu wanaofanya biashara bila kufuata utaratibu ili kukuza sanaa ya filamu nchini na wanaofanya kazi hiyo wakapata heshima katika jamii yao kuliko na kutukuza kazi za nje.
Waziri Nape akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kumaliza hiyo operesheni ya uharamia wa kazi sanaa
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (katikati) akiwa ameambatana na Mkurugenzi wa Idara ya Habari - MAELEZO, Dkt. Hassan Abbas (kushoto) pamoja na maafisa wa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA), wakia katika oparesheni maalum ya kushtukiza la kukamata wafanyabiashara wanaodurufu kazi mbalimbali za sanaa nchini, katika eneo la Karikoo jijini Dar es salaam leo.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (kushoto) akiongoza msafara huo wa kufanya oparesheni maalum ya kushtukiza la kukamata wafanyabiashara wanaodurufu kazi mbalimbali za sanaa nchini, katika eneo la Karikoo jijini Dar es salaam leo. Picha na Iman Nsamila.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akiangalia baadhi ya DVD feki zilizokuwepo katika moja ya maduka ya Kariakoo, Jijini Dar es salaam leo.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akiingia katika moja ya stoo za Duka mojawapo linalouza na kudurufu kazi za wasanii mbalimbali nchini.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...